Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Fahamu Dalili 10 za saratani ambazo watu wengi hawazitambui kirahisi

Dalili 10 za saratani ambazo hazitambuliwi kirahisi

Fahamu; Watu wengi, wanaposikia neno Kansa au saratani, huhusisha na ugonjwa hatari Zaidi na wenye matokeo mabaya ikiwemo kusababisha KIFO.

Ukweli ni kwamba tangu miaka ya 70, kiwango cha kuishi kimeongezeka kwa sababu mbali mbali ikiwemo utambuzi wa mapema wa Saratani.

Saratani ni Ugonjwa mbaya na unaweza kusababisha Kifo ikiwa umechelewa kuugundua na kuanza Tiba mapema, ila ukiwahi unapata matibabu na kupona kabsa,

Aina nyingi za Saratani zinaweza kutibiwa na matokeo yakawa mazuri kwa mgonjwa ikiwa zimegunduliwa kabla hazijakua sana au kufikia hatua|Stage mbaya.

Tatizo ni kwamba mara nyingi, kwa sababu hatutaki kumsumbua daktari au kutowapa umuhimu wa kutosha, tunapuuza baadhi ya dalili ambazo zinaweza kuwa muhimu kwa uchunguzi wa mapema.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la Cancer Research UK, zaidi ya nusu ya Waingereza kwa wakati fulani wamekumbwa na moja ya dalili zinazoweza kuashiria uwepo wa saratani, lakini ni asilimia 2% tu walidhani wanaweza kuugua ugonjwa huo na zaidi ya theluthi moja ilipuuza kabisa dalili na haikwenda kabsa kwa daktari.

Katriina Whitaker, mtafiti katika Chuo Kikuu cha London na mwandishi mkuu wa utafiti huo, alisema: “Watu wanadhani hatupaswi kuwahimiza kuwa na shauku kujua hali za afya zao, lakini tuna shida na watu ambao wanaona aibu kwenda kwa daktari kwa sababu wanaamini kwamba watapoteza muda na kupoteza rasilimali za mfumo wa afya bila manufaa.

“Tunatakiwa kutuma ujumbe kwamba ukiwa na dalili ambazo haziondoki, hasa zile zinazoonekana kuwa ni dalili za tahadhari, usipuuze, nenda kwa daktari kutafuta msaada,” alisema.

Hizi ni Dalili 10 za jumla za saratani ambazo kulingana na Jumuiya ya Saratani ya Amerika hupaswi kupuuza;

1. Kupungua uzito bila sababu

Watu wengi walio na saratani hupoteza uzito wakati fulani.

Unapopoteza uzito au kupungua uzito bila sababu yoyote, inaweza kuashiria tatizo la kiafya.

Fahamu kwamba; Kupungua uzito kwa kilo 5 au zaidi inaweza kuwa ishara ya kwanza ya saratani.

Hii hutokea mara nyingi zaidi katika aina za Saratani kama vile;

  • Saratani ya kongosho,
  • Saratani ya tumbo,
  • Saratani ya umio,
  • au Saratani ya mapafu.

2. Kupata Homa

Hii huweza kuwa dalili ya maambukizi mbali mbali au magonjwa mengi, Na hata kwa mgonjwa wa Saratani huweza kutokea pia

Homa ni ya kawaida sana kwa wagonjwa walio na saratani, ingawa hutokea mara nyingi zaidi baada ya saratani kuenea kutoka pale ilipoanzia.

Karibu kila mtu aliye na saratani atapata homa wakati fulani, haswa ikiwa saratani au matibabu yake yataathiri mfumo wa kinga.

homa inaweza kuwa ishara ya mapema ya aina mbali mbali za saratani, kama vile;

  • Saratani ya Damu(leukemia)
  • au lymphoma.

3. Kupata Uchovu sana wa Mwili

Kuwa na Uchovu mwingi ambao hauishi hata baada ya kupumzika,Inaweza kuwa dalili ya saratani inayoendelea.

Hata hivyo, katika saratani nyingine, kama vile Saratani ya damu, uchovu unaweza kutokea mwanzoni.

Baadhi ya saratani kama vile ya utumbo mpana(colon cancer) au tumbo zinaweza kusababisha upotezaji wa damu ambao hauonekani wazi,Hii ni njia nyingine ambayo saratani inaweza kusababisha uchovu.

4. Kupata Mabadiliko ya ngozi

Pamoja na saratani ya ngozi, saratani nyingine zinaweza kusababisha mabadiliko ya ngozi ambayo yanaweza kuonekana.

Ishara na dalili hizi ni pamoja na:

  • Kuweka weusi kwenye ngozi (hyperpigmentation)
  • Ngozi na macho kuwa na manjano (jaundice)
  • Uwekundu wa ngozi (erythema).
  • Ngozi Kuwasha
  • Ukuaji wa nywele kupita kiasi n.k

5. Mabadiliko ya tabia ya tumbo au kufanya kazi kwa kibofu

Kufunga choo, kuharisha, au mabadiliko katika umbo la kinyesi chako kwa muda mrefu inaweza kuwa ishara ya saratani ya utumbo mpana maarufu kama Saratani ya koloni.

Kwa upande mwingine, maumivu wakati wa kujisaidia haja ndogo, damu kwenye mkojo, au mabadiliko katika utendaji wa kibofu cha mkojo (kama vile kujisaidia zaidi au kidogo, kujisaidia mara kwa mara n.k) yanaweza kuhusishwa na saratani ya kibofu cha mkojo au Figo.

6.  Kupata shida ya Vidonda visivyopona

Watu wengi wanajua kwamba uvimbe ambao hukua, kuumiza au kuvuja damu unaweza kuwa dalili za saratani ya ngozi, lakini pia tunapaswa kuwa waangalifu kwa majeraha madogo ambayo hayaponi kwa zaidi ya wiki nne.

Kidonda cha mdomo ambacho hakiponi kinaweza kuwa kwa sababu ya saratani ya mdomo.

Mabadiliko yoyote katika kinywa chako ambayo hudumu kwa muda mrefu yanapaswa kuchunguzwa mara moja na daktari.

Vidonda kwenye uume au uke vinaweza kuwa dalili za maambukizi mengine au saratani ikiwa kwenye hatua ya awali, na vinapaswa kuchunguzwa na mtaalamu wa afya.

7. Kupata tatizo la Kutoka damu

Kwa upande mwingine, ikiwa damu inaonekana kwenye kinyesi (ambayo inaweza kuwa na rangi nyeusi sana) inaweza kuwa ishara ya saratani ya utumbo mpana(colon cancer) au saratani ya puru.

Pia Saratani ya shingo ya kizazi inaweza kusababisha kutokwa na damu kusiko kwa kawaida ukeni.

Lakini pia, kukojoa mkojo wenye damu inaweza kuwa ishara ya saratani ya kibofu au figo,

Kutokwa na damu kwenye chuchu kunaweza kuwa ishara ya saratani ya matiti(breast cancer) n.k

8. Kuwa na Ugumu au uzito mahali popote kwenye mwili

Fahamu Saratani nyingi zinaweza kuhisiwa kupitia ngozi,

Saratani hizi hutokea hasa kwenye matiti, tezi dume, tezi (lymph nodes), na tishu laini za mwili.

uzito au ugumu unaweza kuwa ishara ya mapema ya saratani.

9. Kupata Ugumu wa kumeza Kitu

Kupata tatizo la ugumu wa kumeza kitu inaweza kuwa dalili za saratani ya umio (mrija unaoelekea kwenye tumbo), Saratani ya tumbo, au koromeo (koo).

Hatahivyo, kama ilivyo kwa dalili nyingi kwenye orodha hii, Tatizo hili huweza kuwa dalili ya matatizo mengine ya kiafya mbali na saratani.

10. Kikohozi cha kudumu au sauti ya kukwaruza

Kuwa na tatizo la Kikohozi cha kudumu inaweza kuwa ishara ya saratani ya mapafu.

Unashauriwa kumtembelea daktari ikiwa umekuwa ukiugua kwa zaidi ya wiki tatu.

Wakati huo huo, sauti ya kukwaruza inaweza kuwa ishara ya saratani ya zoloto (sehemu ya mwanzo ya koromeo) au saratani ya tezi.

KWA USHAURI ZAIDI, ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.