Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wawakikishi wa wamiliki wa vituo vya Afya nchini ambao ni watoa huduma za NHIF

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amekutana na wawakikishi wa wamiliki wa vituo vya Afya nchini ambao ni watoa huduma za NHIF kwa lengo la kujadili Kitita cha Mafao kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kuwa na makubaliano ya pamoja na kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa wanachama nchini.

Waziri @ummymwalimu amekutana na watoa huduma hao wa NHIF leo Januari 4, 2024 katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya zilizopo Jijini Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Waziri Ummy amewataka wawakikishi hao kujadiliana na kutoa maoni yao kwa uwazi na kwa kutanguliza maslahi mapana ya Watanzania ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wananchi bila kikwazo cha fedha.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu, Mwenyekiti wa APHFTA Dkt. Egina Makwabe, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Bw. Juma Muhimbi, Mfamasia Mkuu wa Serikali Bw. Daud Msasi na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Bw. Bernard Konga.

Pia, wawakilishi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) pamoja na wawakilishi kutoka Bohari ya Dawa (MSD).

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.