Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya kuongeza makalio,Janga kwa Wanawake wengi hivi Sasa

Madhara ya kuongeza makalio,Janga kwa Wanawake wengi hivi Sasa.

Fahamu ukweli wa mambo kuhusu hili la kuongeza Makalio,

Kwa hivi Sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la Watu kurekebisha maumbile yao ikiwemo kuongeza Makalio pasipo kufahamu madhara yake.

Na watu hutumia njia mbali mbali ikiwemo dawa,Sindano na hata kufanya Upasuaji ili kufikia Lengo hili la Kuongeza Makalio.

Je,Unafahamu Madhara ya Kuongeza Makalio?

Wataalam wengi wa afya ikiwemo wa kwenye kitengo cha Upasuaji wameelezea madhara mbali mbali ya kuongeza Makalio kwa njia mbali mbali kama vile; kutumia dawa,Sindano, au kufanya Upasuaji.

Mfano; Njia ya Sindano(Buttock injections) ni mojawapo ya njia maarufu ya kuongeza Makalio kwa Wanawake wa nchi kama Venezuelan ili kuwa na muonekano wa kuvutia kwenye Jamii Zao,

Sindano hizi zimetengenezwa kwa kutumia biopolymer silicone, ambapo zina uwezo wa kupenya moja kwa moja ndani ya mwili pasipo kuzuiwa na kitu chochote, hali ambayo hufanya kuwa hatari Zaidi kwa afya.

Silicone ina uwezo wa kuhama na kusambaa sehemu zingine za mwili kwani haiwezi kuzuiwa na kitu chochote mwilini. Pia Kinga ya mwili kwa Mhusika aliyetumia huweza kuonyesha matokeo(react immunologically) ili kupambana na kitu kilichoingizwa mwilini na hapa ndipo madhara makubwa Zaidi hutokea.

Hili limethibitishwa na Wataalam mbali mbali wa afya ikiwemo daktari bingwa wa Upasuaji(Daniel Slobodianik, cosmetic surgeon).

Mgonjwa huweza kuanza kupata allergic reactions na uchovu wa kudumu mwilini(chronic fatigue), na endapo kiambata hiki kitasambaa maeneo mengine ya mwili huweza kusababisha maumivu makali ya Joints.

Madhara ya kuongeza makalio

Kwa Mujibu wa jarida linalohusika na Upasuaji yaani “Plastic Surgery” haya hapa ni Madhara ambayo unaweza kuyapata wakati wa kuongeza Makalio;

– Hatari ya kupata Tatizo la ganzi isiyoisha maeneo mbali mbali mwilini

– Kupata tatizo la kuvuja damu(hematoma)

– Kupata tatizo la Viungo vyako kutofautiana ukubwa

– Kupata matatizo ya damu kuganda, magonjwa ya moyo, mapafu n.k(Deep vein thrombosis, cardiac and pulmonary complications)

– Kupata tatizo la Tisu aina ya Fatty tissue kuoza na kufa(fat necrosis),

Hapa ndipo mtu huanza kupata matokeo kama vile Kuoza Makalio n.k

– Kupata tatizo la maji kujaa na kujikusanya sehemu moja-Fluid accumulation (seroma)

– Kuwa kwenye hatari Zaidi ya kupata maambukizi ya magonjwa

– Kupata hali ya kuchoma choma, ganzi na maumivu ambayo hayaishi.

– Kuanza kupata tatizo la kidonda kuchelewa kupona

– Ngozi kuanza kulika, kunyonyoka na kupotea

– Kupata kovu ambalo haliishi daima n.k

Wengine baada ya Upasuaji huweka Butt implants ambapo ni kifaa chenye lengo la kuongeza ujazo kwenye makalio.

Pia madhara Zaidi ya kuongeza Makalio yameelezewa na jarida laAmerican Society for Aesthetic Plastic Surgery”

ambapo wao wamelezea Zaidi kwa wale wanaofanya Upasuaji wa Kuongeza Makalio;

Haya ni baadhi ya madhara yaliyoorodheshwa kwa wanaoongeza Makalio;

  1. Kuvuja damu kupita kiasi baada ya Upasuaji
  2. Kupata maumivu makali ambayo hayaishi
  3. Kupata kovu
  4. Ngozi kunyonyoka, kuvimba n.k
  5. Kuoza kwa tisu za Makalio
  6. Maji kujaa kwenye eneo la Makalio
  7. Damu kujikusanya eneo moja chini ya makalio
  8. Kupata tatizo la Mzio(allergic reactions)
  9. Ngozi kupoteza rangi yake ya asili
  10. Kuanza kupata shida ya kichefuchefu

Hitimisho;

Hayo ndyo baadhi ya Madhara ya kuongeza makalio….!!!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.