Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya red eyes, haya ni madhara ya Ugonjwa wa macho mekundu

Madhara ya red eyes, haya ni madhara ya Ugonjwa wa macho mekundu

Je, yapi ni Madhara ya red eyes? Baada ya ugonjwa wa macho mekundu(red eyes) kushamiri, moja ya Swali ambalo tumekuwa tukiulizwa sana ni kuhusu Madhara ya red eyes,

Hivo basi, kupitia Makala hii utapata majibu ya Swali hili la “Madhara ya red eyes”, Soma Zaidi hapa…!!!!

Madhara ya red eyes:

Madhara ya red eyes yanategemea na chanzo chake na jinsi ugonjwa ulivyokuathiri Zaidi,

Kuna sababu kadhaa za ugonjwa wa macho mekundu. Hapa kuna baadhi zinazojulikana zaidi, ikiwa ni pamoja na ukali wao na jinsi tunavyozishughulikia.

Soma Zaidi hapa: Chanzo cha Ugonjwa wa Red eyes(macho mekundu)

Sababu za ugonjwa wa Red eyes ni nyingi mno, mfano unaweza tu kuingiwa machoni na uchafu,particles(pollen),vumbi n.k vikakusababishia shida ya macho mekundu,

Ingawa pia matatizo kama vile mzio(allergy) pamoja na maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile Virus n.k, huweza kusababisha ugonjwa wa red eyes.

Kama ni uchafu tu au kitu chochote kimeingia kwenye macho, kikitolewa nje unakuwa sawa au unaweza kuosha macho utakaa sawa, Na ikiwa una shida ya Mzio(allergy) utapewa dawa jamii ya antihistamine ili kutibu tatizo lako.

Na kama umepata ugonjwa wa red eyes baada ya kuvimba mishipa ya damu machoni kutokana na ugonjwa kama vile presha ya macho(glaucoma), huweza kusababisha madhara zaidi ikiwemo kupoteza uwezo wa macho yako Kuona na hilo ni tatizo kubwa Zaidi ambalo linahitaji Msaada wa haraka.

Bahati Nzuri ni kwamba; Asilimia kubwa ya Sababu za ugonjwa wa red eyes hazisababishi Madhara makubwa mwilini.

Ingawa, ikiwa una ugonjwa wa red eyes halafu unapoteza uwezo wa macho kuona vizuri, hii inaweza kuathiri shughuli zako za kila siku ikiwemo;

  • Kupika
  • Kuendesha gari n.k

Hali hii inaweza kusababisha madhara Zaidi ikiwemo Watu kuumia kutokana na ajali(Vision impairments in these areas can result in accidental injury).

Hali zingine za macho ambazo hazijatibiwa zinaweza kusababisha uharibifu wa kudumu kwa jicho, ambapo inaweza kusababisha Macho kupoteza uwezo wake wa Kuona,

Mifano ya hali kama hizi ni pamoja na maambukizi ya macho(eye infections), presha ya macho(angle-closure glaucoma) pamoja na kupata majeraha ya macho au kuumia kwenye macho.

Kwa asilimia kubwa, Madhara ya red eyes ni Pamoja na;

  • Kuvimba kwa Macho(conjunctivitis)
  • Uharibifu wa macho(superficial corneal injury)
  • Ingawa wakati mwingine Red eyes huweza kuwa Ishara ya matatizo makubwa zaidi kama vile; Presha ya machoho(acute angle glaucoma), matatizo kama iritis, keratitis au scleritis n.k.
  • Kupata maumivu
  • Kupata tatizo la Macho kukimbia mwanga(photophobia)
  • Kupungua kwa uwezo wa macho kuona n.k

Ikiwa hakuna Vifaa Maalum vya Uchunguzi wa macho, Mtaalam wa afya atafanya maamuzi kulingana na dalili zinazoonekana kwa mgonjwa,

Moja ya maamuzi hayo ni; Kumpa mgonjwa referral kwenda kwa wataalam wa macho(Ophthalmologist) kwa ajili ya uchunguzi Zaidi.

Matibabu ya Ugonjwa wa red Eyes

Matibabu au Dawa ya Redeyes hutegemea na chanzo husika,

Soma Zaidi hapa; Kuhusu Matibabu au dawa ya Kutibu red eyes.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.