Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA JIPU KWENYE JINO(dalili na Tiba yake)

  JIPU

• • • • •

TATIZO LA JIPU KWENYE JINO(dalili na Tiba yake)


Moja ya majipu ambayo husumbua sana watu ni pamoja na jipu ambalo hutokea eneo la kwenye Jino.


DALILI ZA JIPU HILI NI PAMOJA NA;


– Mtu kupata maumivu makali ya jino ambayo husambaa kwenye taya zima,fizi pamoja na shingoni


– Kupata maumivu makali ya jino wakati wa kutafuna kitu


– Kupata maumivu makali ya jino wakati wa baridi au joto


– Kuvimba kwenye fizi, ambapo kwa wakati mwingine uvimbe kuonekana hadi kwenye shavu


– Mtu kuvimba uso mzima


– Kuvimba kwa tezi za shingoni au Lymph nodes


– Joto la mwili kuwa juu au maumivu ya jino ambayo huambatana na mtu kuwa na Homa


– Harufu mbaya kuanza kutoka kinywani

N.k


CHANZO CHA SHIDA HII YA JIPU KWENYE JINO


• maambukizi ya Bacteria ambayo huingia moja kwa moja kwenye jino pamoja na mishipa ya damu na fahamu ndani ya jino, hivo kuleta madhara mbali mbali kama Tatizo hili la Jipu.



MATIBABU YA SHIDA HII YA JIPU KWENYE JINO


– Zipo njia mbali mbali za kutibu shida hii kama vile;


Kufanyiwa upasuaji mdogo, Kung’oa jino lililoathiriwa pamoja na matibabu ya dawa mbali mbali jamii ya Antibiotics.



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.