Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA ALLERGY YA MAZIWA(chanzo,dalili na Tiba)

 MAZIWA

TATIZO LA ALLERGY YA MAZIWA(chanzo,dalili na Tiba)

Baadhi ya watu hupata shida mbali mbali baada ya kunywa maziwa au kwa lugha nyingine wana Allergy na maziwa, Tatizo hili hutokea sana hasa kwa watoto wadogo.

Maziwa hayo huweza kuwa maziwa ya Ng’ombe,mbuzi,kondoo n.k

DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;

– Mtu kuwa na vipele kwenye ngozi baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na hali ya kuchomwa chomwa pamoja na kuwashwa sana kwenye lips za mdomo au ndani ya mdomo  baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na hali ya kutoa sauti kama filimbi wakati wa kupumua baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupata shida ya upumuaji baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na tatizo la kuvimba Lips za mdomo au Ulimi baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na shida ya kukohoa sana baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na tatizo la kuharisha baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na tatizo la kichefuchefu na kutapika sana baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na hali ya kuvimba pua ambayo hujulikana kwa kitaalam kama Runny nose baada ya kunywa maziwa

– Mtu kupatwa na hali ya macho kutoa machozi yenyewe baada ya kunywa maziwa

N.k

CHANZO CHA TATIZO HILI

Chanzo kikubwa ni mfumo wa kinga ya mwili yaani Body Immune system kuona maziwa kama kitu cha kigeni kinachoingia mwilini,hivo kupambana nacho.

WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA SHIDA HII

✓ watoto wadogo

✓ Wenaopata allergy juu ya vitu vingine

✓ Wenye matatizo kwenye ngozi mfano ngozi kuvimba,kama vile Atopic Dermatitis

✓ Wenye watu wanaopata shida hii kwenye familia

MATIBABU YA TATIZO HILI LA ALLERGY YA MAZIWA

• Tiba sahihi ya shida hii ni mtu kuepuka kunywa maziwa pamoja na vitu vyote vyenye maziwa ndani yake.

Japo baada ya mtu kupatwa na hali hii huweza kupewa dawa mbali mbali kwa ajili ya Allergy kama vile Cetrizine n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.