MTOTO WA KIKE NI KAWAIDA KUPATA NA HAYA BAADA YA KUZALIWA
MTOTO WA KIKE NI KAWAIDA KUPATA NA HAYA BAADA YA KUZALIWA
Wengi wanashangaa Au kushituka Juu ya Hili.
Ila Inatokea na ni kawaida kabisaaa.
Mtoto anapokuwa tumbon na mada akizaliwa Tu, anakuwa na homon za Mama mwilin mwake yaan kwenye mfumo wake wa Damu,homon kama ya Prolaction inayokuwa imeaongeza mama akiwa na mimba mtoto akizaliwa wengine huwazaliwa na Viziwa au wakizaliwa tu vinaanza kuongezeka??(ni kazi za homon zinazokuwa mwilin mwake),
Lakin Pia homon za Mimba zinazofanya pia wanawake watoke Uchafu chafu mweupe uken,watoto wengine zinawafanya na Uken Kwao kutoa viuchafu HIVYO wakizaliwa.
Lakin pia Mtoto akizaliwa Homon za mama kama estrogen zikiwa zinapungua mwilin(sudden drop off of mothets Estrogen hormone) kwenye mwili wa mtoto kuanzia siku ya 2 mpaka siku ya 10,hufanya mtoto apate vi DAMU UKEN,tunaita FALSE MENSES,au NEONATAL VAGINA BLEEDING,na mtoto anaweza pata tu bleed huto kwa siku 2 mpaka hata 4(sio damu nying za kuvalishana na kubadilisha ma pampus mara kwa mara) ni vidamu kidogo Tu.
Na muhimu yanavyotokea haya yote,Wanawake yaan wamama wengi Huogopa sana,sisi kama wataalamu,Tuna assure tu na kukuelimisha kuwa ni kawaida na ni hali za mpito hazihitaji Tiba,homon za mama nikiisha mwilin kwa mtoto hali zote Hizi,HUPOTEA KABISA..
Mara ya kwanza nikiwa mwanafunzi chuoni, enzi zileeee mwee,niliona wodin katoto kachanga kanatoa uchafu wa maziwa maziwa, nilishangaa na kuwaza mtoto kapata wapi FANGASI….??????,kumbe ni hali tu ya kawaida…
Cc:Uzazipoint #afyaclass
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.