Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
afyatipsMagonjwamagonjwa ya wanaumemagonjwa ya wanawakemagonjwa ya watoto

FAHAMU KIPIMO CHA ULTRASOUND NA UJAUZITO

FAHAMU KIPIMO CHA ULTRASOUND NA UJAUZITO

◾ Kipimo cha ultrasound ni uchunguzi unaotolewa kwa wajawazito wengi kabla ya kujifungua. Kinatumia mawimbi ya sauti kuonyesha picha ya mtoto aliyeko tumboni. Kipimo hichi kinamsaidia mtoa huduma kuangalia afya na ukuaji wa mtoto aliye tumboni.

.

.

◾ Kipimo cha ultrasound kinamsaidia daktari kuona kama kuna tatizo katika ogani, mishipa na tishu bila kufanya upasuaji.

.

Tofauti na tekinolojia nyingine, ultrasound haitumi mionzi, ndio maana ni njia inayopendekezwa kwaajili ya kuangalia ukuaji wa kijusi kipindi cha ujauzito. Wakati wa kufanya kipimo cha ultrasound ni muhimu sana kwa wajawazito wengi- ni mara ya kwanza unapoweza kumuona mtoto wako. Unaweza kuona mikono, miguu na sehemu nyingine za mwili kulingana na lini kipimo kitachukuliwa na mkao wa mtoto wako tumboni. Utaweza pia kujua jinsia ya mtoto wako.

.

.

◾ Wanawake wengi wanafanya kipimo cha ultrasound katika kipindi cha pili cha miezi mitatu ya ujauzito (second trimester) wiki 18-20 ya ujauzito. Baadhi wanafanya katika kipindi cha kwanza cha miezi mitatu ya ujauzito (kabla ya wiki ya 14 ya ujauzito). Idadi ya vipimo vya utrasound na muda unaweza tofautiana kwa wanawake wenye aina fulani ya matatizo ya kiafya kama asthma na kisukari.

.

.

✍ Kuna Tofauti Gani Kati ya Kipimo cha Ultrasound na X-ray?

.

.

Ultrasound inatumia mawimbi ya sauti na mwangwi kutoa picha hai, kama video.

.

X-rays ni njia rahisi na haraka kwa mtaalamu wa afya kutumia kuona viungo vya ndani ya mwili na hali ya mifupa. X-rays zinatumia mionzi kupiga picha ya ogani za ndani ya mwili, na mionzi hiyo ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu.

.

.

◾ Kwanini kipimo cha Ultrsound Kinafanyika?

.

.

Vipimo hivi vitampatia mama mtarajiwa nafasi ya kumuona mtoto wake ambaye hajazaliwa. Lakini pia kipimo hichi kina kazi nyingine.

.

Daktari wako atakutaka ufanye kipimo hich kama utakua na maumivu, kuvimba au dalili nyingine itakayo hitaji uchunguzi wa ogani za ndani ya mwili. Ultrasound inaweza kuangalia sehemu za mwili kama vile: kibofu cha mkojo, ubongo (wa mtoto), macho, figo, ini, ovari, bandama, uterasi, korodani, na mishipa ya damu. 

Cc.afyasolution

#afyaclass

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass