Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA

DAMU KUGANDA

• • • • • •

DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA


Dalili za tatizo la damu kuganda huweza kuonekana kwenye maeneo mbali mbali ya mwili kama vile mikononi,miguuni, kwenye mapafu, kwenye moyo n.k

 

Wakati damu imeganda(Blood clots) kwenye mishipa ya vein miguuni au mikononi hali ambayo hujulikana kwa kitaalam kama deep vein thrombosis (DVT) ni hatari kwani clots za damu huweza kusafiri moja kwa moja kwenda kwenye moyo au mapafu.


Na sana sana damu kuganda maeneo kama haya hutokana na mtu kukaa sehemu moja kwa muda mrefu,kutokutembea kwa sababu mbali mbali kama vile ugonjwa wa miguu, upasuaji n.k


DALILI ZA TATIZO LA DAMU KUGANDA


1). Miguuni au Mikononi


– Mikono au miguu kuvimba na hii huanza kuonekana pale tu damu inapoanza kuganda


– Rangi ya ngozi mikononi au miguuni kubadilika na kuwa Nyekundu zaidi au Blue, na baadhi ya watu huanza kupatwa na miwasho ya ngozi maeneo haya


– Maumivu ya miguu au mikono ambayo huongezeka kadri siku zinavyosogea mbele


– Ngozi ya sehemu ambapo damu imeganda au tatizo la deep vein thrombosis (DVT)  limetokea huwa ya moto zaidi kuliko sehemu zingine


– Misuli ya miguu kuanza kukakamaa(lower leg muscle cramps)


– Uvimbe miguuni ambao huambatana na maumivu ya miguu n.k


2). Mapafu


Kama zile clots za damu baada ya kuganda zimefika kwenye mapafu hali ambayo hujulikana kama pulmonary embolism ni hatari sana kwa mgonjwa,  na mgonjwa huweza kuanza kupata dalili hizi hapa;


– Kupata shida sana ya kupumua au kukosa hewa


– Mgonjwa kuanza kukohoa sana, wengine hukohoa hadi damu


– Kuanza kupata maumivu makali ya kifua wakati wa kupumua


– Kupatwa na kizunguzungu kikali


– Kutokwa na jasho sana mwilini n.k


3). Moyo


– Mgonjwa kupata maumivu makali ya kifua pamoja na mikono


– Mgonjwa kutokwa sana na jasho mwilini


– Kupata shida wakati wa kupumua au kupumua kwa shida


– Kuwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa shambulio la moyo yaani Heart attack

 N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.