Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

SUKARI NYINGI CHANZO CHA UBOVU WA MENO

SUKARI NYINGI CHANZO CHA UBOVU WA MENO

Ulaji wa sukari nyingi au vitu vyenye sukari nyingi huweza kuwa chanzo cha kuharibu meno yako au chanzo cha ubovu wa meno,

Ukipenda kula vitu vya sukari nyingi ambavyo huacha mabaki ya sukari mara kwa mara kwenye meno yako,

usipokuwa mwangalifu na kusafisha kinywa chako kwa mswaki na dawa mara tu baada ya matumizi ya vitu hivo,

Huweza kuanza kuleta madhara kwenye meno yako,

Hii hutokana na nini?

Ukila sukari au vitu vya sukari sana;

Bacteria wa kinywani huvunja ile sukari na kutengeneza Tindikali au acid ambayo sio salama sana katika afya meno.

Lakini pia mabaki yale ya sukari kwenye meno yako,huweza kuwa chanzo kizuri cha Bacteria kuzaliana na kuongezeka,

kisha kuanza kushambulia fizi zako pamoja na meno yako

Wataalam wa afya wanashauri kusafisha meno yako au kupiga mswaki na dawa sio tu wakati wa asubuh,ila na baada ya mlo,

Hii itasaidia kuondoa mabaki ya vyakula na kunyima mazingira ya bacteria kuzaliana.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.