Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KANSA YA MRIJA WA NYONGO au Bile duct cancer kwa Kitaalam CHOLANGIOCARCINOMA

 KANSA

• • • • •

KANSA YA MRIJA WA NYONGO au Bile duct cancer kwa Kitaalam CHOLANGIOCARCINOMA


Kansa hii hushambulia eneo la Mrija wa nyongo(bile duct) uliopo ndani ya Ini ambao unaunganisha kati ya kifuko cha nyongo yaani Gall bladder na Utumbo mdogo.


CHANZO CHA KANSA HII YA MRIJA WA NYONGO(bile duct cancer)


• Kansa hii hutokea pale ambapo kumetokea mabadiliko makubwa ya seli yaani MUTATIONS hali ambayo hupelekea seli kukuwa kuliko kawaida baada ya ukuaji wa seli kushindwa kudhibitiwa.


Lakini pia, kuna sababu mbali mbali ambazo huongeza uwezekano wa mtu kupata aina hii ya Kansa, Kama vile;


✓ Uvutaji wa Sigara


✓ Umri kuwa mkubwa yaani zaidi ya Miaka 50


✓ Mashambulizi ya vimelea Mbali mbali vya Magonjwa kwenye Ini kama vile PARASITE jamii ya LIVER FLUKE


✓ Kuwa na hitilafu kwenye Mrija wa nyongo wakati mtoto anazaliwa


✓ Mtu kuwa na magonjwa sugu ya Ini Au magonjwa ya Ini yanayomsumbua kwa Muda mrefu


✓ Ugonjwa wowote ambao huweza kusababisha mrija wa nyongo kukakamaa na kuwa mgumu zaidi au kutengeneza na kuacha kovu kwenye mrija wa nyongo, Mfano tatizo la SCLEROSING CHOLANGITIS

n.k


DALILI ZA KANSA YA MRIJA WA NYONGO AU BILE DUCT CANCER NI PAMOJA NA;


1. Mgonjwa kupata maumivu makali ya tumbo


2. Ngozi ya mwili na macho kubadilika rangi na kuwa Manjano hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama JAUNDICE


3. Mtu kujisaidia kinyesi ambacho kina rangi nyeupe na sio ile rangi yake ya kawaida


4. Mtu kuchoka kupita kiasi


5. Uzito wa mwili kushuka kwa kasi sana


6. Mtu kupata miwasho ya mara kwa mara kwenye ngozi ya mwili au mtu kuwashwa mwilini



MATIBABU YA KANSA HII YA MRIJA WA NYONGO AU BILE DUCT CANCER


– kansa hii huhusisha matibabu ya Aina mbali mbali kama vile;


• Upasuaji


• Huduma ya mionzi au Radiaotherapy


• Huduma ya Chemotherapy


• Pamoja na mtu kubadilishwa Ini yaani kwa kitaalam LIVER TRANSPLANT


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.