Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

NAMNA MAWE KWENYE KIBOFU HUGUNDULIKA

NAMNA MAWE KWENYE KIBOFU HUGUNDULIKA

Mawe pamoja na matatizo mengine ya mfumo wa ini na nyongo kama nilivyokwisha kusema hapo awali

kunakua hakuna dalili hasa kama ugonjwa haujawa mkubwa au jiwe likiwa halitembei.

Watu wengi wenye mawe kwenye kibofu cha nyongo huja kujua wana mawe pale ambapo wanafanyiwa vipimo vingine vya tumbo na kwa bahati mbaya wanajijua wana tatizo la mawe.

Aidha kwa magonjwa yeyote ya tumboni na hasa hasa kwenye mfumo wa ini na nyongo kipimo kizuri sana cha kuanza nacho na kinachotoa majibu kamili ni kipimo cha atrasaundi (Ultrasonography).

Kutokana na hali ya mgonjwa daktari anaweza kufanya vipimo vingine ili kuona ukubwa wa tatizo,au kama kuna ugonjwa mwingine na pia katika kupima ukubwa wa madhara yaletwalo na uwepo wa mawe kwenye kibofu nyongo,

vipimo ambavyo hupimwa baada ya Ultrasound ili kupima Zaidi ni kama vipimo vya damu kama lipase,amylase, sodium,potasium, AST,ALT, bilirubin, calcium albumin

na vipimo vya choo ili kuchunguza au kubaini kisababishi kingine cha maumivu ya tumbo,

Vile vile vipo vipimo vingine kama CT scan ya tumbo (Abdominal computed tomography (CT),

na MRI ya mfumo wa nyongo na kongosho (magnetic resonance cholangiopancreatography MRCP).

ITAENDELEA…..

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.