Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

IJUE LEBA(KITENDO CHA MWANAMKE KUJIFUNGUA)

IJUE LEBA(KITENDO CHA MWANAMKE KUJIFUNGUA)

LEBA ni matukio yaliyo katika mpangilio yanayotokea kwenye njia ya uzazi ya mwanamke kwa dhumuni la kutoa mtoto alieko tumboni (katika mji wa mimba) kuja duniani kupitia uke.

Maumivu ambayo utafusirika kama uchungu ambayo utokea katika muda maalumu na ambayo huongeza kasi na nguvu/ukali kadri muda unavyoenda na ambayo hutokea chini ya kitovu na utapakaa kwenda mgongoni na mapajani na ambayo huambatana na kutokwa na ute ute ulochanganyikana na damu ni miongoni mwa dalili za leba.

Leba sahihi ni ile ambayo haina changamoto kwa mama wala mtoto, hutokea yenyewe pasipo usaidizi, utokea ikiwa mimba imetimia na ni ile ambayo mtoto utanguliza kichwa.

Maumivu/uchungu wakati wa leba hutokana na kunywea au kukakamaa kwa mji wa mimba ili kusukuma mtoto na inachangiwa na homoni na vichocheo mbalimbali.

Kwa kawaida leba imegawanyika katika hatua kuu tatu

1. Hatua ya kwanza huusisha kufunguka kwa njia ili kuruhusu mtoto kutoka. Hii hatua uhusisha kufunguka kwa shingo ya kizazi yan seviksi ili kuruhusu mtoto kupita. Kwa mwanamke ambaye hajawahi kuzaa hii hatua huweza kuchukua hata masaa 12 na kwa wale ambao wamewahi kuzaa huchukua takribani masaa sita.

2. Hatua ya pili huusishwa kuzaliwa kwa mtoto. Hatua hii huanza mara baada ya kukamilika kwa kufunguka kwa njia na hutimilika baada ya kuzaliwa kwa mtoto. Katika hatua hii nguvu ya utashi wa mama husaidia kusukuma mtoto ili atoke ikisaidiana na minyweo ya mji wa mimba. Kwa mwanamke ambaye hajawahi kuzaa hatua hii inaweza kuchukua hata masaa 2 na kwa ambaye amewah kuzaa inaweza chukua nusu saa.

3. Hatua ya tatu huusishwa kuzaliwa au kutoka kwa kondo la nyuma. Hatua hii huanza baada ya kuzaliwa kwa mtoto na hutimilika baada ya kutoka kwa kondo la nyuma. Hatua hii inaweza kuchukua dakika 5 mpaka 15.

Iwapo nguvu ya kusukuma itakuwa ndogo, kutokuwiana kwa kichwa cha mtoto na njia, mlalo mbaya wa mtoto na changamoto mbalimbali katika nyonga haya huweza kupelekea changamoto wakati wa kujifungua na inawezekana usaidizi ukahitajika. By Dr.Emanuel

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.