Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KILA MARA KAMILISHA DOSE KAMILI YA DAWA(Ushauri)

KILA MARA KAMILISHA DOSE KAMILI YA DAWA(Ushauri)

Kila mara kamilisha dozi kamili ya dawa kama ulivyoandikiwa na daktari.

Unaweza kutumia dawa na baada ya siku chache ukajisikia nafuu,lakini haimaanishi kuwa umepona.

Usipokamilisha dozi vimelea vinakuwa havijadhibitiwa kabisa katika mwili wako.

Kukamilisha dozi kamili husaidia kukulinda wewe, familia yako na jamii

dhidi ya magonjwa yanayoweza kukaa muda mrefu sababu ya vimelea sugu lakini pia hupunguza gharama za matibabu.

Upinzani wa AMR?

Usugu wa vimelea dhidi ya dawa
hutokea pale ambapo vimelea vya
magonjwa hubadilika na kuwa sugu
dhidi ya dawa.

Vimelea ambavyo vinakuwa sugu dhidi
ya dawa vinajumuisha bakteria, virusi,
fangasi, na parasaiti, mfano mbu.

Hali hii hupelekea dawa kushindwa
kufanya kazi ya kuua au kuzuia ukuaji
wa vimelea hivyo kama ilivyokusudiwa.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.