Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA FIZI KUACHANA NA MENO NA KUTENGENEZA UWAZI/NAFASI(DIASTEMA)

TATIZO LA FIZI KUACHANA NA JINO NA KUTENGENEZA UWAZI/NAFASI(DIASTEMA)

Tatizo la meno kuwa na uwazi au kuachana kutokana na Fizi kutengeneza nafasi hujulikana kama Diastema,

Tatizo hili huweza kuwapata watu wazima vijana pamoja na watoto,

Japo kwa baadhi ya watoto shida hii huisha yenyewe pale ambapo wanaanza kuota meno ya kudumu yaani permanent teeth.

Uwazi huu kwenye meno huweza kuwa mdogo sana kiasi kwamba mhusika mwenyewe ndye huona tofauti,

au unaweza kuwa mkubwa sana kiasi kwamba kila mtu anagundua tofauti iliyopo

CHANZO CHA TATIZO HILI LA DIASTEMA

– Hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa tatizo hili,japo kuna baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupatwa na tatizo hili kama vile;

• Meno kuwa madogo sana kuliko size ya Teeth jaw Bone

• Sababu za kigenetics au vinasaba kwenye familia zetu

• kuwa na uvimbe kwenye fizi za meno au kukuwa kwa tissues sehemu ya juu ya meno

• Watoto kuwa na tabia ya kunyonya sana dole gumba kwa muda mrefu,hii huweza kutengeneza nafasi

• Tatizo la Incorrect swallowing reflexes ambapo ulimi wako huenda kinyume na meno yako ya mbele wakati wa kumeza kitu,kitaalam hujulikana kama Tongue thrust

• Magonjwa ya fizi yaani Gum diseases

• Matumizi mbalimbali ya kemikali kwenye meno kwa lengo la kusafisha,au urembo kwenye meno.n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.