Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUPATA HEDHI KWA MUDA MREFU

TATIZO LA KUPATA HEDHI KWA MUDA MREFU

Tunasema mwanamke ana tatizo la kupata hedhi kwa muda mrefu hasa pale ambapo inachukua zaidi ya siku 7 au wiki moja.

Hivo basi,Mwanamke ambaye anapata hedhi mfululizo zaidi ya siku 7 au zaidi ya wiki, yupo kwenye kundi la wanawake wenye tatizo la kupata hedhi kwa Muda mrefu.

CHANZO CHA TATIZO LA KUPATA HEDHI KWA MUDA MREFU

Zipo baadhi ya sababu mbali mbali ambazo huchangia uwepo wa tatizo hili,na sababu hizo ni kama vile;

1. Mabadiliko ya vichocheo mwilini(hormone changes), Mwanamke huweza kubata mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini kutokana na sababu mbali mbali kama vile;

• Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama sindano,vidonge n.k

• Matumizi ya Emergence contraceptives maarufu kama P2 mara kwa mara

• Mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini kipindi cha balehe(puberty) au karibu na kufikia ukomo wa hedhi yaani Perimenopause

• Matatizo kama thyroid disorders or polycystic ovary syndrome. n.k

2. Mabadiliko kwenye utokaji wa yai yaani Ovulation changes, Kama Ovaries zako hazitoi mayai kipindi cha hedhi, basi ukuta mzito hujengwa kwenye mji wa mimba,

Ambapo wakati ikifikia hatua ya kubomoka yaani Uterine thick line sheding ndipo mwanamke hupata period kwa muda mrefu sana kuliko kawaida.

3. Matumizi ya dawa mbali mbali kama vile;

– Matumizi ya njia za uzazi wa mpango kama sindano,vidonge n.k

– Matumizi ya Emergence contraceptives maarufu kama P2 mara kwa mara

– Matumizi ya aspirin, anti-inflammatories,pamoja na blood thinners nyingine

4. Ujauzito, sio period kama period nyingine,lakini wakati mwingine unaweza kuendelea kuvuja damu ukiwa mjamzito kumbe ni mimba inatishia kutoka, au tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

5. Tatizo la uvimbe kwenye kizazi yaani(Uterine fibroids ,Adenomyosis or polyps), Tatizo hili pia huweza kusababisha mwanamke kupata period kwa muda mrefu zaidi.

6. Tatizo kwenye tezi la Thyroid, unaweza kuwa na tatizo la kublid kwa muda mrefu kutokana na kutokufanya kazi vizuri kwa thyroid gland hali ambayo kwa kitaalam hujulikana kama hypothyroidism

7. Hali ya damu yako mwenyewe, hapa nazungumzia vitu kama uwezo wako wa damu kuganda,hemophilia n.k

Kama una tatizo hili la damu kutokuganda unaweza kupata blid mfululizo kwa muda mrefu sana.

8. Tatizo la Obesity, Watu wengi hawajui kwamba kuwa na uzito mkubwa kupita kawaida(Excessive body weight) huweza kuchangia mwanamke kupata period kwa muda mrefu zaidi.

Hii ni kwa sababu ya FATTY TISSUE huweza kusababisha mwili wako kuzalisha zaidi kichocheo cha Estrogen,hali ambayo huweza kuleta mabadiliko kwenye mzunguko wako wa hedhi.

9. Maambukizi ya bacteria kwenye via vya uzazi vya Mwanamke yaani Pelvic inflammatory disease (PID), Tatizo hili huweza kusababisha mwanamke kuanza kutokwa na uchafu ukeni,period nyeusi,na blid kwa muda mrefu pia.

10. Tatizo la kansa/Saratani ya kizazi au Saratani ya shingo ya kizazi, kwa baadhi ya Wanawake wenye Saratani hizi huweza kuanza kupata period kwa muda mrefu zaidi kuliko kawaida kama dalili za mwanzoni kabsa za Saratani hizi.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.