Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MAGONJWA YA MACHO AMBAYO HUWAPATA WATU WENGI ZAIDI

MAGONJWA YA MACHO AMBAYO HUWAPATA WATU WENGI ZAIDI.

Haya hapa ni baadhi ya magonjwa ya macho ambayo huwapata watu wengi zaidi.

1.Ugonjwa wa Presha ya macho ambayo kwa kitaalam hujulikana kama Glaucoma.

SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa presha ya macho(Glaucoma)

2. Ugonjwa wa mtoto wa jicho au kwa kitaalam hujulikana kama Cataract.

Ugonjwa huu huhusisha uwepo wa kitu kama wingu kwenye lensi za macho, na ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza duniani kwa kusababisha Upofu wa macho.

SOMA HAPA ZAIDI: Ugonjwa huu wa mtoto wa jicho(Cataract)

3. Ugonjwa wa vikope maarufu kama Trakoma, kujua zaidi ugonjwa wa VIKOPE au TRAKOMA

SOMA HAPA: Ugonjwa wa vikope au Ugonjwa wa TRAKOMA,chanzo,dalili na Tiba yake

4. Ugonjwa wa RED EYES.

SOMA ZAIDI HAPA: ugonjwa wa RED EYES,chanzo,dalili na Tiba yake

5. Tatizo la Diabetic Retinopathy, shida hii hutokana na ugonjwa wa kisukari, ambapo ugonjwa huu wa kisukari huleta madhara makubwa hadi kwenye mishipa ya damu ndani ya Retina,

Na ndyo maana baadhi ya wagonjwa wa kisukari wanapatwa na tatizo la macho kutokuona vizuri pia.

6. Tatizo la Refractive Errors, ambapo huhusisha shida ya kuona karibu yaani myopia (near-sightedness), shida ya kuona mbali yaani hyperopia (farsightedness), pamoja na tatizo la macho kutokuona vizuri mbali wala karibu yaani astigmatism (distorted vision at all distances).

7. Tatizo la Age-Related Macular Degeneration, ambapo tatizo hili la macho hutokana na umri mkubwa au uzee,

8. Tatizo la Amblyopia au kwa lugha nyingine hujulikana kama Lazy Eye, Tatizo hili la macho huaathiri zaidi uwezo wa kuona kwa watoto wadogo,

Na tatizo hili hutokana na macho pamoja na Ubongo kutokufanya kazi vizuri kwa kushirikiana hali ambayo hupelekea uwezo wa kuona kwa jicho moja kupungua sana,

Na wakati mwingine tatizo la Cataract pamoja na Strabismus huchangia pia uwepo wa shida hii.

9. Tatizo la Strabismus, tatizo hili huhusisha kutokuwa na uwiano(imbalance) kwenye kuposition macho yako mawili.

Na tatizo hili hutokana na kukosa coordination kati ya macho yako mawili, na matokeo yake macho yako mawili huangalia kwenye direction tofauti, badala ya macho yote mawili kufocus kwenye kitu kimoja, kila jicho hutazama upande wake.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.