Dawa ya minyoo Albendazole,ifahamu vizuri dawa hii
Dawa ya minyoo Albendazole,ifahamu vizuri dawa hii,
Generic name yake: Albendazole Tablets na Albendazole oral suspension
Dawa hii dose yake ipo kwenye mfumo wa vidonge yaani Tablets pamoja na mfumo wa suspension(kimiminika/syrup)
– Kidonge kimoja(tablet) kina Albendazole USP 200mg, pamoja na zingine zina USP 400mg
– Albendazole suspension ina 5mls, sawa na Albendazole USP 200mg,
Dawa hii ya Albendazole ipo kwenye therapeutic Category:PO2-Anthelmintic
Njia ya matumizi ya dawa hii au Route of administration ni kupitia mdomoni yaani Oral route.
MATUMIZI YA ALBENDAZOLE(INDICATIONS)
• Dawaa hii ya Albendazole hutumika kutibu tatizo la Minyoo,
dawa hii huweza kutibu single au Mixed Infections ya;
– Enterobius Vermicularis
– Trichuris trichiura
– Ascaris Lumbricoides
– Ancylostoma duodenale
– Necator Americanus
– Strongyloides stercoralis
– Taenia spp. Capillariasis
– Cysticercosis n.k
TAHADHARI;Warnings
Dawa za Albendazole hazitumiki kwa Mama mjamzito au Mwanamke ambaye anategemea kubeba mimba kwa kipindi hicho,
Pia tahadhari nyingine ni kuhusu blood counts na Liver function tests kabla ya matibabu, pamoja na kwa mama anayenyonyesha(breastfeeding),
Weka dawa hizi mbali na watoto-Keep the medicine out of reach of children.
MADHARA(SIDE EFFECTS) YA DAWA HIZI
– Kwa wagonjwa ambao wana heavy Intestinal infection wanaweza kupata maumivu ya tumbo na kuharisha,
– Kupata hali ya kizunguzungu kwa baadhi ya watu
– Kupata maumivu ya kichwa kwa baadhi ya watu
– Na kwa wale ambao wanajioverdose huweza kupata shida ya Bone marrow depression, Leucopenia,Pancytopenia n.k
HAYO NDYO BAADHI YA MAELEZO MACHACHE KUHUSU DAWA HII YA ALBENDAZOLE.