Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Muda sahihi wa Unyonyeshaji(wiki ya unyonyeshaji duniani)

Tukiwa bado kwenye wiki ya Unyonyeshaji Duniani ambayo ilianza Aug ust 1-7, zipo dondoo mbali mbali tutaendelea kushare na wewe kuhusu Swala zima la Unyonyeshaji bora,

Leo tunagusia kuhusu kipindi au muda sahihi wa unyonyeshaji;

Wataalam wa afya hupendekeza kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza, ambapo kwa kitaalam hujulikana kama “Exclusive breastfeeding”

Mtoto anatakiwa kunyonyeshwa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha bila kumchanganyia na kitu kingine chochote,

Baada ya hapo utaanza kumchanganyia na vitu vingine, lakini usiache kumnyonyesha maziwa yako mpaka atakapofikisha umri wa miaka miwili au zaidi kama ukiweza.

Shirika la Afya Duniani(WHO) linapendekeza #kunyonyesha maziwa ya mama pekee kwa miezi sita ya kwanza ya maisha, na kuendelea kunyonyesha kwa miaka miwili au zaidi, ikiwa wazazi wanaweza kufanya hivyo.

WHO recommends exclusive #breastfeeding for the first six months of life, and continued breastfeeding for two years or beyond, if parents are able to do so.

#WikiyaUnyonyeshajiDuniani

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.