Dalili hizi huweza kuashiria Shida kwenye Mapafu
Dalili hizi huweza kuashiria Shida kwenye Mapafu,
– Mtu kupata maumivu makali ya kifua
– Mtu kuanza kukohoa kikohozi kikavu sana
– Mtu kukosa pumzi au kupata shida sana wakati wa kupumua
– Mtu kushindwa kupumua kwa urahisi yaani Orthopnea mpaka awe amesimama ndyo hupata unafuu n.k
NB: Orthopnea ni hali ya mtu kushindwa kupumua akiwa amelala chini(lying down),
Hii hutokea sana kwa watu wenye matatizo ya moyo pamoja na Mapafu
Hizi ni Dalili za matatizo mbali mbali ambayo huhusisha Mapafu, kama vile shida ya kujaa maji kwenye mapafu yaani kwa kitaalam PLEURAL EFFUSION n.k
Hivo ukipata dalili kama hizi Nenda hospital Kufanya VIPIMO zaidi.