Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Upungufu wa nguvu za kiume,chanzo,Dalili na Tiba yake

Upungufu wa nguvu za kiume,chanzo,Dalili na Tiba yake

TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME,CHANZO,DALILI NA TIBA

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume huweza kuhusisha; Uume kushindwa kabsa kusimama, uume kutokusimama kwa muda mrefu, Kukosa nguvu ya kuanza au kuendelea na tendo n.k

hali ambazo hupelekea mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake ambaye anashiriki naye tendo la ndoa kwa wakati huo.

CHANZO CHA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Zipo sababu nyingi sana ambazo huchangia wanaume kuwa na tatizo hili la Kukosa nguvu za kiume, na baadhi ya sababu hizo ni pamoja na;

– Mtindo mzima wa maisha kwa mwanaume ikiwemo ulaji wake wa kila siku

– Mwanaume kuwa na magonjwa ya moyo ambayo huweza kuathiri usafirishaji wa damu mwilini

– Uwepo wa kiwango kikubwa cha lehemu yaani High cholesterol unaweza kusababisha tatizo la uume kushindwa kusimama vizuri(erectile dysfunction)

– Tatizo la kuwa na kiwango kidogo cha hormones za kiume yaani Low testosterone Level

– Tatizo la Clogged blood vessels (atherosclerosis)

– Ugonjwa wa presha ya kupanda yaani High blood pressure huweza kuleta effect mpaka kwenye mfumo wa uzazi

– Ugonjwa wa kisukari(Diabetes),huweza kuathiri uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa ikiwemo tatizo hili la uume kushindwa kusimama vizuri yaani erectile dysfunction

– Tatizo la Uzito kuwa mkubwa yaani Overweight/Obesity, Mwanaume mwenye uzito mkubwa sana,Bonge n.k anaweza kushindwa kufanya vizuri hata kwenye tendo la ndoa.

Hivo unashauriwa kuhakikisha unazuia tatizo hili la uzito kuwa mkubwa/kupita kiasi.

– Tatizo la Metabolic syndrome, ambalo huhisisha vitu hivi kwa ujumla wake; Presha kuwa kubwa zaidi,Level ya Insulin kuwa kubwa sana,Mafuta ya mwili(Body fat) kuzidi pamoja na kiwango cha cholestrol kuwa kikubwa zaidi.

– Matatizo mengine kama vile;Parkinson’s disease,Multiple sclerosis n.k pia huweza kuleta athari kwenye mfumo wa uzazi

– Uvutaji wa Sigara ikiwemo matumizi ya Tumbaku(Tobacco)

– Matumizi ya baadhi ya Dawa kama vile dawa jamii ya antidepressants, antihistamines,dawa za kutibu presha(high blood pressure), maumivu au matatizo ya tezi dume

– Unywaji wa Pombe kupita kiasi pamoja na aina nyingine za ulevi au madawa ya kulevyia

– Ugonjwa wa Peyronie’s disease, ugonjwa huu huhusisha kutokea na kuendelea kwa kovu(Scar tissues) ndani ya Uume

– Tatizo la kukua kwa tezi dume(enlarged prostate),kansa/Saratani ya Tezi Dume(prostate cancer) pamoja na Matibabu yake

– Mwanaume kuumia au kupata majeraha kwenye maeneo ya via vyake vya uzazi ikiwemo kwenye nyonga pamoja na uti wa mgongo

– Mwanaume kufanyiwa upasuaji kwenye eneo la nyonga(Pelvic) au uti wa mgongo(Spinal cord)

– Tatizo la msongo wa mawazo,hofu,wasi wasi pamoja na matatizo mengine ambayo huhusisha afya ya akili(mental health problems),Vitu hivi huweza kuleta athari mpaka kwenye uwezo wako wa kufanya tendo la ndoa.

– Migogoro ya kila mara kwenye mahusiano yako ambayo pia huweza kuleta tatizo la msongo wa mawazo au stress,wasi wasi,hofu n.k

– Pia tafiti zinaonyesha kadri Mwanaume anavyokuwa na umri mkubwa(mzee) ndivo na nguvu zake za Kiume huendelea kupungua sana ikiwemo uwezo wa uume kusimama vizuri na kwa muda mrefu.

– Baadhi ya matatibu kama vile;Upasuaji wa Tezi Dume(prostate surgery) au huduma ya mionzi(radiation treatment) kwa wagonjwa wa kansa pia huweza kuathiri uwezo wa tendo kwa mwanaume

– Pamoja na Sababu zingine…

DALILI ZA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

• Uume kushindwa kusimama kabsa

• Uume kutokusimama vizuri

• Uume kusimama ila sio kwa muda mrefu

• Mwanaume kushindwa kurudia tendo, goli moja chali hawezi tena kurudia tendo

• Mwanaume kuwahi kufika kileleni na kushindwa kabsa kuendelea

• Kukosa kabsa hisia au hamu ya kufanya tendo la ndoa n.k

MADHARA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME NI PAMOJA NA;

✓ Mwanaume kushindwa kumridhisha mwenza wake wakati wa tendo la ndoa

✓ Kuongeza wasi wasi,woga na hofu kubwa ya kufanya mapenzi kwa Mwanaume

✓ Mwanaume kutokujiamini tena

✓ Mwanaume kukosa kabsa hamu ya kufanya tendo la ndoa

✓ Kuanza migogoro kwenye mahusiano au ndoa,kusalitiana n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.