Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

NJIA ZA UZAZI WA MPANGO,MADHARA YAKE NA NJIA SAHIHI KUTUMIA

 

?ZIFAHAMU NJIA ZOTE ZA UZAZI WA MPANGO NA NJIA SALAMA KULIKO ZOTE

☑️ SUMMARY

kwanza Njia za Uzazi wa Mpango zimegawanyika katika Makundi yafuatayo;
     
       (a) Kuna Njia za asili au Tradition methods Mfano; KALENDA
       (b) Kuna Njia za kisasa au Modern methods Mfano; Vipandikizi
 
Lakini pia Hizi za Kisasa tunaweza kuzigawanya zaidi katika Makundi yafuatayo;
 
(1) Njia za Mda Mfupi Mfano; Kondom za kike na za Kiume pamoja na Vidonge
 
(2) Njia za mda Mrefu Mfano; Vipandikizi au Njiti za miaka 3 na 5, Lupu au kitanzi cha miaka 10-12
 
(3) Njia za kudumu Mfano; Kufunga uzazi kwa mwanaume au mwanamke

NJIA ZOTE ZA UZAZI WA MPANGO NA MAELEZO YAKE

(1) KALENDA
 
Njia hii ni salama kwa asilimia mia moja(100%)  kwa mtumiaji japo kuna angalizo; Kama mzunguko wako wa hedhi haubadiliki badiliki basi njia hii inafaaa kwako, japo asilimia kubwa ya wanawake mizunguko yao ya hedhi hubadilika badilika hivo ni rahsi sana kupata Ujauzito wakitumia Njia hii.
 

?Hitimisho: Kalenda ni Njia bora na salama ya Uzazi wa Mpango ila kwa mtu ambaye Mzunguko wake wa hedhi haubadiliki badiliki yaani ni STABLE MENSTRUAL CYCLE

(2) KONDOM ZA KIUME NA KIKE
 
Hii pia ni Njia ya Uzazi wa Mpango salama na Nzuri kwani Ina faida mara mbili (i) Kuzuia mimba (ii) Kukukinga na Magonjwa ya Zinaaa kama Kaswende,Ukimwi n.k
 
Japo pia Wengi husema Hupunguza ladha ya Tendo la Ndoa.
 
(3) VIDONGE VYA MAJIRA
 
Njia hii huhusisha mtumiaji kumeza kila siku kidonge kimoja kimoja,na endapo ataacha au kusahau hata siku moja,yupo kwenye hatari ya Kupata Mimba au Ujauzito
 
Kutokana na vichocheo vilivopo katika Njia hii ya Uzazi bas Kuna maudhi madogo madogo huweza kumpata Mtumiaji kama vile; kuumwa na kichwa sana,kupata kichefuchefu na kutapika n.k

Hitimisho: Njia hii sio nzuri kwa Mtu ambaye anapanga Uzazi kwa mda mrefu kama miaka 2 au 3, kwani itamlazimu kumeza vidonge kila siku na kwa Mda mrefu

(4) SINDANO
 
Njia hii huhusisha uchomaji wa Sindano maarfu kama DEPO-INJECTION na haya ni maelezo kwa kina Juu ya Madhara ya athari za Sindano. ?
 
 

⚠️ MADHARA YA SINDANO ZA UZAZI WA MPANGO

Je Wajua kwamba sindano za uzazi wa mpango zinaweza; 

✓ kukusababisha ukakaa mda mrefu bila kubeba mimba Yaani kitaalam huitwa LONG INFERTILITY

✓kulainisha mifupa yako ya mwili?

✓zinaweza kuvuruga kabsa mzunguko wako wa hedhi? ikiwemo kukusababisha usipate kabisa hedhi kwa mda mrefu au kupata damu nyingi ya hedhi na kublid kwa mda mrefu pia?

✓Maumivu makali ya kichwa,kichefu chefu,na kutapika

(5) NJITI/KIPANDIKIZI

kuna Njiti ya Miaka 3 na vile vya Miaka 5

Njia hii pia ina vichocheo ndani yake hivo,ni rahsi kwa mtumiaji kupata madhara yafuatayo;

* Kuumwa na kichwa sana pamoja kizunguzungu

* Kubalika kabsa kwa Mzunguko wa hedhi yaani IRREGULAR MENSTRUAL CYCLE,kupata blid kama vitone tone bila kukata au kutoka kwa mda mrefu,Kupata damu nyingi ya Hedhi na kwa mda mrefu mfano zaidi ya wiki moja.

* Kupatwa na kichefuchefu pamoja na Kutapika

 

 MAUDHI AU MADHARA YA MATUMIZI YA NJITI/KIPANDIKIZI KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO

 

➡️ Ombeni Mkumbwa

 
Ukweli ni kwamba,kwa,asilimia kubwa Njia za uzazi wa Mpango ambazo zina vichocheo ndani yake huleta mabadiliko makubwa katika mwili wa Mtumiaji.
Mfano; Njia ya vidonge vya Majira,Sindano,Njiti au vipandikizi zote hizi ni aina za Njia za Uzazi wa Mpango zenye vichocheo ndani yake.
 
LEO TUNAZUNGUMZIA BAADHI YA MADHARA AU MAUDHI MADOGO MAGODO YA KUTUMIA NJITI KAMA NJIA YA UZAZI WA MPANGO.
 
Kuna kijiti cha Miaka 3 Na kuna vile vya Miaka 5, Vyote hivi ni aina ya Vipandikizi au Njiti.
 

(1)Kublid vitone vitone alafu kwa mda mrefu

 
(2)Kuwa na mzunguko wa hedhi unaobadilika badilika,Hapa tunaamanisha kitaalam kama Irregular Menstrual cycle Mfano; Mwezi huu umeona period yako siku ya 28,mwezi unaofata 21,Mwezi mwingine 33.Yaani hakuna Mpangilio maalumu unaoeleweka
 
(3)Maumivu makali ya kichwa,hili pia huweza kumpata mwanamke mtumiaji wa Njia hii Mara kwa Mara
 
(4)Kujisikia vibaya na kutapika pia
 
(5)Kukonda sana au kunenepa Sana
 
(6)Kublid damu nyingi na kwa Mda mrefu pia
 
(7)Kuchelewa kupata Ujauzito baada ya kuacha kutumia Njia hii.
 
(8)Kukaa mda mrefu bila Mwanamke kuona Siku zale
 
NB: SIO KILA NJIA YA UZAZI WA MPANGO NI MBAYA, mfano kalenda ni Njia ya Uzazi zuri sana kwa Mwanamke ambaye Mzunguko wake wa Hedhi haubaliki badiliki,Mfano kama ni Siku 28, ni hizo hizo siku zote. Cha muhimu ni upate Elimu ya kutosha Juu ya Mzunguko huu
 
ANGALIZO
 
Tafiti zinaonyesha Wanawake wengi huchagua njia flani za Uzazi wa Mpango kutokana na ushaur au ushawishi wa Mafariki,Ndugu,Jamaa,Majirani au Watu wanaowazunguka sio kutokana na Ushauri wanaopewa na Wataalm wa afya,Alafu wakija kupata Madhara wanalalamika.
 
NI VIZURI KWENDA HOSPTAL AU KUONA WATAALM WA AFYA USHAURIWE NJIA SALAMA INAYOENDANA NA MWILI WAKO.
 

Au pia unaweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255758286584 tutakupa Maelekezo sahihi kwa ajili ya Afya Yako.

 
 

(6) LUPU/KITANZI

Njia hii kwa asilimia kubwa ni safi na salama kwani haihusishi uwepo wa kichocheo chochote ambacho kinaweza kuleta athari kubwa kwa mwili wa Mtumiaji kama vile kuvuruga vichocheo vya mwili yaani Hormone Imbalance n.k.

 

 

KUMBUKA NJIA SALAMA KWAKO INATEGEMEA NA MWILI WAKO SIO USHAWISHI WA NDUGU AU JAMAA,KWAHYO NI MUHIMU KUKUTANA NA WATAALAM WA AFYA MKAJADILI NJIA SAFI NA SALAMA ITAKAYOENDANA NA MWILI WAKO.

NJOO INBOX SAIV KUPITIA NAMBA 0758286584 NIKUSHAURI NJIA SAHIHI YA UZAZI WA MPANGO INAYOENDANA NA MWILI WAKO.

 

P2 NI NINI? NA MADHARA YAKE NI YAPI?

➡️ Ombeni Mkumbwa

 p2 ni dawa ya dharura (emergency contraceptive),inazuia mtu asipate Mimba kwenye mazingira ambayo umefanya sex pasipo kupanga na upo siku za hatari,au umelazimishwa kufanya sex au umebakwa,ili kuzuia mimba zisizotarajiwa unalazima Kunywa hizi dawa

 

P2-Ni Dawa iliyotengenezwa kutumiwa mara chache tu,inapokulazimu.Sio dawa unayotakiwa kutumia kama njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu. Kuna wanawake humeza p2 kila mwezi,hii haitakiwi. Katika mazingira ya kawaida,haipaswi kumezwa zaidi ya mara 3 kwa mwaka. Kuendekeza kila mwezi kunywa hizi p2 sio sahihi,Unatakiwa ende hospitali ili upate njia sahihi ya uzazi wa mpango ya muda mrefu.

 

 

Baadhi ya Side effects/madhara ni ya matumizi holela ya dawa hizi ni 

1.Unaweza kujisikia kichefuchefu au kutapika baada ya kumeza,

2.Maumivu ya tumbo

3.Matiti kuuma na kujaa 

4.Pia hedhi zako zinazofuata zinaweza zikawahi au zikachelewa au zikatoka nyingi sana( ukiona zimezidi siku 8 fika muone daktari) au ukawa unapata hedhi nyepesi sana,au pia haupati hedhi kabisa (amenorhoea)

5.Kichwa kuuma na kizunguzungu

6.Mabadiliko ya Ute ukeni (change in cervical secretion,hapa unakuta Ute wa ovulation mtu hapati).

7.Kupata maambukizi ukeni,vaginal infections

8.Hatari ya kupata PID

9.Maumivu wakati wa sex(dyspareunia)

10.Mama anakuwa hatarini kutungisha mimba nje ya kizazi yaani ectopic pregnancy.

11.Lakini pia kuna wanawake hupata Ovarian cyst,vivimbe kwenye mfuko wa mayai.

Kuna sababu hapo juu kama PID,kutopata UTE,infections kwenye uke hizi zinakuja athiri mwanamke anakuwa anapata taabu kwenye Kupata mimba

Kama hujapanga kupata mimba,tafadhari fuata njia ya uzazi wa mpango ya muda mrefu inayokufaa,achana na kumeza p2 kila mwezi. 

Follow us on INSTAGRAM: @afyacheck_

Karibu Sana..!!

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.