Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DALILI ZA UTI KWA WOTE(MWANAMKE NA MWANAUME)

DALILI ZA UTI KWA WOTE(MWANAMKE NA MWANAUME)

Katika makala hii,nmekupa baadhi ya dalili ambazo ukiziona zinatokea kwenye mwili wako,

unaweza kuwa na maambukizi ya kwenye njia ya Mkojo au UTI

KUMBUKA; UTI ni kifupi cha maneno haya “Urinary tract Infection”

Hapa tunazungumzia maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama vile bacteria,

ambayo huhusisha mfumo wa mkojo ikiwemo;Njia ya mkojo,kibofu cha mkojo,Figo N.k

Unaweza kupata maambukizi ya bacteria kwenye Njia ya Mkojo(UTI) ambayo hujirudia mara kwa mara yaani recurrent infections,

Tatizo la UTI Sugu,UTI ambayo haiishi au UTI ambayo hujirudia rudia mara kwa mara huweza kusababisha madhara zaidi,ikiwemo;

  • Kusababisha tatizo la Uke kuwa Mkavu zaidi kwa Mwanamke
  • Kuathiri mzunguko wa hedhi
  • Kupelekea matatizo mengine kama PID,wakati bacteria wakipenya na kuingia kwenye via vya uzazi vya mwanamke n.k

DALILI ZA UTI KWA WOTE(MWANAMKE NA MWANAUME) NI PAMOJA NA;

-Kupata maumivu makali ya nyonga,

– Kupata maumivu ya mgongo,

– Kupata maumivu ya joint pamoja na viungo mbali mbali vya mwili

– Kupata maumivu ya tumbo hasa hasa upande wa kushoto

– Kuhisi kukojoa mara kwa mara ila ukikojoa mkojo haushi

– Kuhisi hali ya kuchoma wakati wa kukojoa

– Kukojoa mkojo wenye rangi kama pink au nyekundu,hii ni baada ya UTI kuwa ya mda mrefu na kuanza kuleta madhara makubwa

– Kuhisi hali ya uume kuwaka Moto

– Kuhisi hali ya kuchoma au kuwasha kwenye tundu au njia ya mkojo

– Kupata uchovu wa mwili kupita kiasi au Mwili kuchoka sana

– Joto la mwili kuwa juu au Mtu kuwa na Homa(Fever)N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.