Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Mpigania Uhuru mwanamke wa Kenya afariki dunia akiwa na miaka 92

Mpigania Uhuru mwanamke wa Kenya afariki dunia akiwa na miaka 92

Mpigania Uhuru wa kike wa Kenya aliyekuwa na cheo cha juu zaidi nchini humo Muthoni wa Kirima (92), amefariki dunia.

Bi.Kirima alikuwa mtu muhimu sana kwenye mapambano ya kupigania Uhuru na Mwanamke pekee aliyepewa cheo cha Field Marshal wakati wa harakati za Mau mau kwenye miaka ya 1950.

Alizaliwa mwaka 1930 na kukulia kwenye mazingira magumu yaliyojaa vurugu za kibaguzi jambo lililomsukuma kuamua kupigania kwa ajili ya Uhuru.

Mwaka 1952 alijiunga na Mau Mau na kuahidi kuwapatia wanachama taarifa. Baada ya muda mfupi alikwenda kuwa mpiganaji wa msituni na aliheshimika sana kwa ujuzi wake wa kupambana.

Rais William Ruto ameeleza kusikitishwa kwake na msiba huo na ametuma salamu za rambirambi kwa familia pamoja na wakenya wote.

“Alikuwa mtu muhimu mwenye mchango mkubwa katika kupigania Uhuru, jasiri na mchapakazi aliyejitoa kwa ajili ya familia yake, jamii na nchi ya Kenya. Tunauheshimu mchango wake wa kishujaa”.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.