Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba yake)

 MALARIA

• • • •

UGONJWA WA MALARIA(chanzo,dalili na tiba yake)

CHANZO CHAKE;

Ugonjwa wa malaria ni ugonjwa ambao husababishwa na Vimelea vya magonjwa ambavyo kitaalam hujulikana kama PLASMODIUM na kusambazwa kwenda kwa mtu na mbu jamii ya ANOPHELES.

Vimelea hivi vya Plasmodium vimewekwa katika makundi mbali mbali kama vile;

1. Plasmodium Oval

2. Plasmodium Vivax

3. Plasmodium Malariae

4. Pamoja na Plasmodium Falciparum

DALILI ZA UGONJWA WA MALARIA NI PAMOJA NA;

– Mgonjwa kupata hali ya kizunguzungu kikali

– Mgonjwa kupatwa na hali ya kichefuchefu pamoja na kutapika

– Mgonjwa kukosa kabsa hamu ya kula chakula

– Joto la mwili kupanda au mgonjwa kuwa na homa

– Kupatwa na maumivu ya kichwa mara kwa mara

– Kupata maumivu ya viungo,misuli pamoja na joint kwenye mwili wako

– Mwili wa mgonjwa kuchoka au kupata uchovu kupita kiasi

– Malaria kali huweza kusababisha mtu kuwa na dalili za kuchanganyikiwa, kuweweseka N.K

– Lakini pia malaria huweza kuleta shida ya upungufu wa damu mwilini, hivo mgonjwa huweza kupata dalili mbali mbali za upungufu wa damu mwilini kama vile;

 macho kubadilika rangi na kuwa meupe au paleness

Ngozi ya kwenye viganja vya mikono, lips za mdomo kuwa nyeupe au paleness

Kukosa nguvu,kizunguzungu N.K

MATIBABU YA UGONJWA WA MALARIA

– Dawa mbali mbali huweza kutumika kutibu ugonjwa wa malaria kama vile; Malaffin,ALU(maarufu kama Mseto), Quinine N.K

 Lakini dawa kama Sulfadoxine Pyrimethamine (SP) huweza kutolewa kwa mama mjamzito kwa ajili ya kumkinga na Ugonjwa wa Malaria.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.