Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la kukosa choo kwa mjamzito au kupata choo kigumu kwa mjamzito

kukosa choo kwa mjamzito au kupata choo kigumu kwa mjamzito

Baada ya mwanamke kubeba mimba moja ya changamoto kubwa ambayo huweza kukutana nayo ni kukosa choo au kupata choo kigumu sana(constipation),

Tatizo hili hutokea kwa wajawazito wengi, na baadhi ya tafiti zinaonyesha karibu nusu ya wanawake wote hupata tatizo hili wakati wa ujauzito.

Chanzo cha Tatizo la kukosa choo kwa mjamzito au kupata choo kigumu kwa mjamzito

Asilimia kubwa,chanzo cha Tatizo la kukosa choo kwa mjamzito au kupata choo kigumu kwa mjamzito hutokana na mabadiliko makubwa ya vichocheo mwilini,

Ingawa baadhi ya sababu zingine huweza kuongeza ukubwa wa tatizo hili, Sababu hizo ni pamoja na;

  • Kuongezeka kwa hofu na msongo wa mawazo
  • Kutokufanya mazoezi au kupunguza shughuli za mwili
  • Kunywa maji kidogo n.k

Vitu vya kufanya kwa Tatizo la kukosa choo kwa mjamzito au kupata choo kigumu kwa mjamzito

fanya mambo haya kama unapata tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu wakati wa Ujauzito;

1. Hakikisha unapata nyuzi nyuzi zaidi, moja ya njia ya kupata nyuzi nyuzi(fibers) ni kula matunda kama parachichi, machungwa n.k

Soma hapa Zaidi, Vyakula anavyostahili kula mama mjamzito

2. Kunywa maji mengi zaidi,

Maji ni muhimu zaidi wakati wowote wa ujauzito, kwani husaidia kupeleka virutubisho muhimu kwa mtoto wako. Zaidi ya hayo, ni muhimu pia kunywa maji ya kutosha ili kuhakikisha kwamba fiber unayokula inaweza kufanya kazi yake na kuweka mfumo wako sawa,

maji husaidia sana kama unapata Tatizo la kukosa choo au kupata choo kigumu wakati wa ujauzito.

3. Fanya Mazoezi, Swala la kuwa mjamzito haimaanishi uwe unalala tu ndani, jitahidi sana kuushughulisha mwili kwa kufanya mazoezi,

Tafiti zinaonyesha Kutembea kwa angalau dakika 10-15 kila siku husaidia mambo kwenda vizuri na kuondoa matatizo kama vile hili la kukosa choo au kupata choo kigumu(constipation).

4. Fanya vitu ambavyo havitakupa msongo wa mawazo, ikiwemo kufanya vitu unavyovipenda zaidi, kufanya mazoezi, kuoga kwa maji ya moto n.k

Soma Zaidi hapa kuhusu shida hii;

KUPATA CHOO KIGUMU KWA MJAMZITO

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.