Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KUPATA CHOO KIGUMU KWA MJAMZITO

KUPATA CHOO KIGUMU KWA MJAMZITO

Wakina mama wengi wajawazito hukumbana na hili tatizo la kupata choo kigumu wakati wa ujauzito au kwa kitaalam constipation.

Je chanzo cha tatizo hili kwa mama mjamzito ni kipi?

Kupata Choo kigumu wakati wa ujauzito husababishwa na baadhi ya misuli ya Tumbo ku relax na kupungua kwa Peristalisis (ile nguvu inayotumika kusukuma chakula kutembea ndani ya matumbo),

na hali hii husababishwa na kichocheo cha progesterone ambacho huzalishwa kwa wingi wakati wa ujauzito

JE NINI KIFANYIKE KAMA HALI HII YA KUPATA CHOO KIGUMU WAKATI WA UJAUZITO IKITOKEA?

Kuepukana na hali fanya baadhi ya mambo haya yafuatayo;

– Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau lita 2.5 mpaka 3 kwa sku

– Kula matunda na mbogamboga kwa wingi

– Usile vyakula vilivyokobolewa kwa wingi

– Kunywa glasi moja ya maji kabla ya chai husaidia Mmengenyo mzuri wa chakula

– Fanya mazoezi usikae tu kwa sababu ni mjamzito,Mazoezi husaidia pia kwenye hali hii hasa mazoezi ya kutembea n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.