Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la kuwashwa sehemu za siri(Wanawake&Wanaume)

Tatizo la kuwashwa sehemu za siri(Wanawake&Wanaume)

Tatizo la kuwashwa ukeni chanzo chake

Via vya uzazi vya mwanamke vimekuwa vikishambuliwa na magonjwa mbali mbali kama Maambukizi katika via vya uzazi yaani PID, Fangasi N.K. Baadhi ya magonjwa yakionyesha dalili mapema wakati mengine yakichelewa.

SABABU ZA KUWASHWA UKENI

Je Kuwashwa Sehemu za Siri kunatokana na nini?

– Dalili za magonjwa mbali mbali kama Fangasi wa Sehemu za siri,

Mfano:Fangasi jamii ya Candida Albicans hushambulia zaidi sehemu za siri na kusababisha dalili mbali mbali ikiwemo hii ya kuwashwa ukeni

– Magonjwa ya zinaaa kama kasendwe,kisonono, au chlamydia,

Pia magonjwa kama haya huweza kuambatana na dalili za kuwashwa Ukeni

– Matumizi ya baadhi ya sabuni zenye makemiko sehemu za siri

– Kuwashwa kutokana na magonjwa ya ngozi

– Kuwashwa kunakosababishwa na allergy ya kitu flani, Mfano nguo za ndani,pedi N.k

– Kushuka kwa kinga ya mwili kutokana na sababu mbali mbali kama Ujauzito au matumizi ya dawa flani,hivo kupelekea sehemu za siri kushambuliwa haraka na magonjwa kama Fangasi,UTI n.k

ZINGATIA MAMBO HAYA MUHIMU KWAKO

Mambo ya kufanya baada ya hali hii ya muwasho kutokea

Fanya usafi wa kutosha mara tu baada ya kukojoa au tendo la ndoa

Zingatia swala la kuweka mazingira ya sehem za siri kuwa safi mda wote

Epuka kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri

Epuka kuvaa nguo za ndani zinazobana

Jitahidi kubadilisha nguo ya ndani mara tu baada ya kuitumia mfano baada ya siku moja

TATIZO LA KUWASHWA KWENYE UUME

Tatizo hili huwasumbua Wanaume wengi, bila kujua chanzo chake na cha kufanya.

Na miwasho hii huweza kusambaa mpaka sehemu ya korodani

CHANZO cha tatizo la Kuwashwa kwenye Uume

Sababu kubwa ya tatizo hili la miwasho kwenye uume ni maambukizi ya Fangasi ambapo kwa kitaalam hujulikana kama Candidiasis au Male Yeast Infection.

Jamii hii ya Fangasi wa CANDIDA ALBICANS hushambulia sana eneo la Sehemu za siri kwa Wanawake na Wanaume pia

DALILI ZA MAAMBUKIZI HAYA

– miwasho kwenye uume

– miwasho kuzunguka eneo lote la korodani na ngozi yake

– ngozi ya korodani kuwa nyekundu zaidi

– kupata miwasho ukeni kwa wanawake

– kutokuwa na uchafu ukeni kama maziwa mgando

– kuwa michubuko pamoja na vidonda sehemu za siri

EPUKA MAMBO HAYA:

– kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka vizuri au zenye unyevu unyevu

– Kuvaa nguo za ndani zenye material ya mpira hasa wakati wa joto kali na jua kali

– N.k

MATIBABU YA SHIDA HII

Tatizo hili hutibika kwa kutumia dawa mbali mbali za Fangasi kama vile; Clotrimazole Cream N.k

Hivo ongea na wataalam wa afya kwa ajili ya msaada wa kimatibabu, kama una tatizo hili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.