Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Saratani ya Tumbo,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Saratani ya Tumbo,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Kuna tofauti kati ya Saratani ya Tumbo na Saratani ya Utumbo, Saratani ya tumbo hutokea kwenye eneo la tumbo(Stomach Cancer) na Saratani ya utumbo hutokea eneo la utumbo mfano; Saratani ya Utumbo mpana(Colon Cancer) n.k

Katika Makala Hii tumechambua Zaidi kuhusu Saratani hii ya Tumbo(Stomach Cancer),chanzo chake,dalili Pamoja na Tiba

CHANZO CHA SARATANI YA TUMBO

Chanzo halisi cha Saratani ya tumbo Hakifahamiki, Ingawa kuna Sababu zenye Uhusiano wa Karibu Sana na tatizo hili la Saratani ya Tumbo,

Moja ya Sababu hizo ni Pamoja na;

• Maambukizi ya Bacteria H. pylori, Bacteria anayesababisha Vidonda vya tumbo,

• Kuvimba kwenye kuta za tumbo yaani gastritis,

• Aina ya Upungufu wa Damu kwa Muda mrefu inayojulikana kama pernicious anemia,

• kuwa na Ukuaji(Growths) kama vile polyps

• Ukuaji Usio wakawaida wa Seli ndani ya Tumbo

• SABABU ZINGINE Ambazo huongeza hatari ya mtu kupata Saratani ya Tumbo;

– Uvutaji wa Sigara

– Kuwa na tatizo la Uzito mkubwa,Unene n.k(overweight/obesity)

– Kula vyakula vyenye chumvi nyingi Mara kwa Mara

– Unywaji wa Pombe Kupita Kiasi

– Kufanyiwa upasuaji wa tumbo kwa ajili ya vidonda tumboni(ulcer)

– Maambukizi ya Virusi kama vile Epstein-Barr virus infection

– Kufanya kazi katika viwanda vya makaa ya mawe, chuma, mbao au mpira

– Kuwa na Historia ya tatizo hili kutokea kwenye Familia yako(genes/genetic factors)

DALILI ZA SARATANI YA TUMBO NI ZIPI?

Dalili za Mwanzoni Kabsa ni Pamoja na;

– Kuhisi tumbo Kujaa baada ya kula chakula

– Kupata Kiungulia mara kwa mara

– Kupata Kichefuchefu kidogo

– Kupoteza hamu ya kula

– Tatizo la Indigestion

KUMBUKA; Kuwa na Dalili hizi haitoshi kusema tayari mtu ana Saratani ya Tumbo, Dalili hizi huingiliana na magonjwa mengine mengi,

Kadri Saratani ya Tumbo inavyoendelea kukua, ndipo Dalili zaidi huanza kuonekana, Mfano wa Dalili zingine ni kama vile;

– Kupata Maumivu makali ya Tumbo

– Kujisaidia kinyesi kimechanganyika na Damu

– Kutapika Mara kwa Mara

– Uzito wa Mwili Kupungua kwa Kasi Pasipo Sababu inayoeleweka

– Kuanza kupata shida wakati Ukimeza kitu

– Macho au ngozi kubadilika rangi na Kuwa Manjano

– Tumbo kuwa kubwa au Kuvimba

– Kupata shida ya Choo Kigumu(Constipation) au Kuharisha Mara kwa Mara(diarrhea)

– Kuhisi uchovu wa Mwili usiowakawaida n.k

VIPIMO:

Hivi ni Baadhi ya Vipimo ambavyo huweza kufanyika kwa Mgonjwa;

• Vipimo vya Damu(Blood tests)

• Kipimo cha endoscopy

• Ct Scan

• Ultrasound

• Kuchukua Kinyama na kwenda kukichunguza yaani Biopsy N.K

MATIBABU YA SARATANI YA TUMBO

Kama ilivyo kwa aina Zingine za Saratani, Kupata Tiba Mapema ndyo Kupona Kabsa, Lakini ukichelewa kupata Tiba na Saratani hii Kufikia Stage 4 ni ngumu zaidi kupata Tiba na Kupona,

Baadhi ya Matibabu yake ni Pamoja na;

– Mgonjwa kufanyiwa UPASUAJI

– Huduma ya chemotherapy

– Huduma ya radiation therapy

– Huduma Ya Chemo na Radiation kwa Pamoja yaani Chemoradiation n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.