Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

KUKOJOA BAADA YA TENDO LA NDOA NA KUZUIA MIMBA AU UJAUZITO

 JE KUKOJOA MARA TU BAADA YA TENDO LA NDOA HUZUIA MWANAMKE KUPATA MIMBA?

➡️ Ombeni Mkumbwa

Kuna Maneno Mengi na Imani Nyingi kwamba Mwanamke akienda kukojoa Chooni Mara tu baada ya Tendo la Ndoa Hupunguza uwezekano wa Kupata Mimba au Ujauzito…

➖ UKWELI; Mwanamke Kukojoa Mara kwa mara hupunguza Uwezekano wa Kupata UTI na wala sio Ujauzito..

Tafiti zinaonyesha kwamba, wakati wa Tendo La Ndoa Mwanaume huweza kuzalisha Mbegu Nyingi Mfano; kati ya Million 20 mpaka 400, na Zaidi ya asilimia 65% ya Mbegu huingia Moja kwa Moja kwenye Mlango wa Uzazi.. . Kumbuka; Mara tu baada ya Mbegu hizo kuzalishwa hukimbilia moja kwa Moja kwa Speed kubwa kuelekea kwenye Mirija ya Uzazi huku zikitafta Yai kulirutubisha.

Mbegu nyingi za kiume hufia Njiani kutokana na Mazingira ya Ndani ya Sehemu za Siri za mwanamke,Lakini pia mbegu nyingi huweza kulifikia Yai,endapo mbegu Moja imefanikiwa kuingia Ndani ya yai.Yai hilo hufunga kabsa na kutokuruhusu Mbegu nyingine kupita.

➖ Hivo basi Kitendo cha kwenda Kukojoa baada ya Tendo la Ndoa, mbegu za Kiume tayari zimeshaingia Ndani Mda Mrefu na zipo tayari kukutana na Yai ili kulirutubisha.

Pia Njia ya Mkojo kupita na Tundu la uke ambapo mbegu za Kiume hupitia Ni tofauti kabisa hivo hata ukikojoa vipi huwezi kutoa mbegu ambazo tayari zimeshaingia Ndani.

NB; Faida Ya kukojoa Mara unapohisi au mara baada ya Tendo la ndoa huweza kukusaidia kuepusha magonjwa kama Uti(Urinary tract Infection) au maambukizi katika Njia Ya Mkojo, Magonjwa ya Figo n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.