Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo La Mimba Kuharibika,chanzo,dalili na Tiba

Tatizo La Mimba Kuharibika

Tatizo La Mimba Kuharibika,chanzo,dalili na Tiba yake,

Katika makala hii tumechambua Zaidi kuhusu Chanzo cha Tatizo La Mimba Kuharibika,dalili za mimba kuharibika pamoja na Tiba yake.

Tatizo La Mimba Kuharibika limekuwa kubwa hasa katika siku za Hivi karibu,na mimba nyingi zinaharibika au kutoka hata kabla ya Kumaliza Miezi mitatu(3) ya mwanzoni,

na asilimia kubwa ya wanawake hawa wenye Tatizo La Mimba Kuharibika wamekuwa wakipata shida ya Ujauzito wa Kwanza kutoka wenyewe,

Zipo sababu Nyingi ambazo husababisha Wanawake wengi kupata tatizo la Mimba Kuharibika Zenyewe kwenye vipindi tofauti tofauti vya Ujauzito

SABABU ZA TATIZO LA MIMBA KUHARIBIKA

Zifuatazo ni Baadhi ya Sababu Zinazochangia Kutokea kwa Tatizo la Mimba kuharibika au kutoka Zenyewe kwenye vipindi tofauti tofauti kwa ujumla wake;

1. Matatizo yanayotokana na Mfumo mzima wa Kijenetiki ambapo kitaalam hujulikana kama-Genetics Abnormalities,

tatizo hili huchangia mimba kuharibika hasa hasa katika kipindi cha Miezi mitatu(3) ya Mwanzoni.

2. Matatizo katika Via vya Uzazi vya Mwanamke kama Vile;

Kulegea kwa shingo ya kizazi hivo kushindwa kuhimili kushikilia ujauzito hatimaye ujauzito kutoka wenyewe n.k

3. Matizo kama Vile Uvimbe kwenye kizazi pia huweza kusababisha Tatizo La Mimba Kuharibika

4. Tatizo la Mvurugiko wa Vichocheo vyako vya Mwili ambapo kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance

5. Uwepo wa Magonjwa mbali mbali kipindi cha Ujauzito kama vile;

  • Ugonjwa wa kisukari,
  • Kifafa cha Mimba,
  • Shinikizo la Damu,
  • Ugonjwa wa Goita
  • Pamoja na maambukizi mengine kama vile ya Rubella n.k.

6. Matumizi ya baadhi ya dawa ambazo ni hatari kipindi cha Ujauzito kama vile,

matumizi ya dawa za Msongo wa mawazo mfano;

  • paroxetine
  • au venlafaxine n.k

7. Kupata ajali, kuanguka,kupigwa eneo la tumboni n.k

Vitu vinavyoongeza hatari ya kupata Tatizo La Mimba Kuharibika

TABIA HATARISHI ZINAZOWEZA KUPELEKEA MWANAMKE KUPATA TATIZO LA MIMBA KUHARIBIKA ZENYEWE NI PAMOJA NA;

– Matumizi ya vilevi kama vile Pombe

– Uvutaji wa Sigara

– Matumizi ya vinywaji venywe Caffeine Nyingi

– Matumizi ya Dawa kiholela au Ovio bila kupewa maelekezo na wataalam wa afya n.k

Dalili za Mimba Kuharibika

Dalili za mimba kuharibika ni pamoja na;

– Kupatwa na Maumivu makali sana ya Tumbo

– Kuanza kublid au kuvuja damu wakati wa Ujauzito

– Damu nyingi kutoka ikiambatana na vipande kama maini au mabonge mabonge n.k

VIPIMO vya Tatizo La Mimba Kuharibika

Ukiwa na tatizo la mimba kuharibika mara kwa mara au ukiwa unapata Dalili hizo za mimba kuharibika ni muhimu zaidi kwenda Hospital ili kupata vipimo mbali mbali kama Vile;

  • ULTRASOUND,
  • vipimo vya Mkojo,
  • Vipimo vya Damu n.k

Hii itasaidia kugundua chanzo cha tatizo lako na kuanza Matibabu mara moja.

MATIBABU ya Tatizo La Mimba Kuharibika

Yapo matibabu mbali mbali kwa Mtu mwenye tatizo hili la mimba kuharibika kama Vile kupewa dawa za kusaidia kutunza Ujauzito,

Kutokufanya kazi zozote nzito na kupata Mapumziko ya Kutosha ambapo kitaalam tunaita BED-REST.

Lakini kama Ujauzito umeshatoka Kuna huduma kama vile kusafishwa hospitalini,kupewa antibiotics kwa Ajili ya kuzuia mgonjwa asipate maambukizi n.k

FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara

Je, Zipi ni dalili za Tatizo La Mimba Kuharibika?

Dalili za mimba kuharibika ni pamoja na;

– Kupatwa na Maumivu makali sana ya Tumbo

– Kuanza kublid au kuvuja damu wakati wa Ujauzito

– Damu nyingi kutoka ikiambatana na vipande kama maini au mabonge mabonge n.k

Hitimisho

Tatizo La Mimba Kuharibika huweza kusababishwa na Sababu mbali mbali ikiwemo; Matatizo yanayotokana na Mfumo mzima wa Kijenetiki ambapo kitaalam hujulikana kama-Genetics Abnormalities, matatizo ya kizazi kama vile Kulegea kwa shingo ya kizazi n.k

Tatizo la Mvurugiko wa Vichocheo vyako vya Mwili ambapo kitaalam hujulikana kama Hormone Imbalance,matumizi ya baadhi ya dawa,maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile; Rubella n.k.

Ni muhumu sana kufahamu kuhusu Dalili za mimba kuharibika ili kupata msaada wa haraka, Dalili za mimba kuharibika ni pamoja na;

Kupata Maumivu makali sana ya Tumbo,Kuanza kublid au kuvuja damu wakati wa Ujauzito,Damu nyingi kutoka ikiambatana na vipande kama maini au mabonge mabonge n.k

KWA USHAURI ZAIDI/ELIMU/TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.