Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MAMBO 10 YAKUZINGATIA KATIKA AFYA YA MWANAMKE

 MAMBO 10 YAKUZINGATIA KATIKA AFYA YA MWANAMKE

(1) Kutokupuuzia Kila dalili za Magonjwa pale zinapotokea

Mfano dalili kama za Kuwashwa sehemu Za siri, Kutokwa na uchafu wenye harufu mbaya ukeni, kupata maumivu wakati wa Tendo la Ndoa,Mkojo kuchoma wakati wa Kukojoa, Kutokuona Hedhi kwa mda mrefu,kutoa usaha na damu kwenye chuchu na dalili zingine zozote.Kwani kila dalili ni kiashiria cha Ugonjwa au Tatizo flani. Hivo ili afya ya mwanamke kuwa salama lazima azizingatie dalili hizi na kupata msaada kwa wataalam wa afya.


(2) Usafi wa ndani na Nje ya mwili.

Usafi wa Nguo,mfano nguo za ndani na za Nje pia, Usafi wa mwili kwa Ujumla


Swala la Usafi ni lazima kwa kila mtu,kwahyo hutakiwi kupuuzia kabsa usafi,maana usipokuwa msafi unatengeneza mazingira mazuri ya kupatwa au kushambuliwa na Magonjwa


(3) Kuchagua Njia sahihi ya Uzazi wa Mpango ambayo inaendana na mwili wako kama Umeamua Kupanga Uzazi

Kwahyo pata ushauri kwa kina kutoka kwa wataalam wa afya juu ya njia gani Salama inayoendana na mwili wako,kama Umeamua kupanga Uzazi. Usichague njia flani ya uzazi kwa sababu umeambiwa,umeshauriwa,umeshawishiwa na ndugu,jamaa,majirani,ndugu,marafiki au kwa vile mwenzako anatumia. 


(4) Kama wewe ni Mjamzito

Nenda kliniki,hakikisha mahudhurio yote manne unahudhuria kwa ajili ya afya yako pamoja na Kiumbe ulichobeba. Hapa namaanisha; 


~ Hudhurio la kabla ya wiki 16 za Ujauzito


~ Hudhurio la wiki 20-24 za Ujauzito


~ Hudhurio la wiki 28-32 za Ujauzito


~ Hudhurio la wiki 36-40 za Ujauzito


(5) Zijue dalili za hatari ukiwa Mjamzito na hata baada ya Kujifungua

Mfano; Kublid wakati wa Ujauzito,kuvimba miguu kupita kiasi,uso na mikono pia, na dalili zingine zote za hatari.


(6) Hakikisha uzito wako wa mwili haupitilizi au hauzidi,

 Soma zaidi hapa..!! afyacheck26.ml


(7) Kutokutumia Dawa hovio bila kupata Maelekezo kutoka kwa Wataalam wa afya

Usipate dalili ya Ugonjwa flani,ukakimbilia kumeza dawa,bila kuongea na wataalam wa afya na ukapewa maelekezo sahihi juu ya aina za dawa sahihi kwako na matumiz yake kwa Ujumla


(8) Hakikisha unakunywa Maji mengi kwa siku ili kuboresha afya yako

Mfano; Tafiti zinaonyesha unywaji wa maji wastani wa Lita 2.5 kwa siku,hupunguza uwezekano wa kupata UTI za mara kwa mara kwa zaidi ya asilimia 50%.


(9) Pata lishe bora hapa namaanisha Balance diet

(10) Omba ushauri au msaada kutoka kwa wataalam wa afya kama una tatizo lolote au kuna kitu unaona hakijakaa sawa katika mwili wako

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KUPITIA NAMBA +255758286584

Karibu Sana..!!!



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.