Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MJAMZITO ANATAKIWA ALALIE UPANDE WA KUSHOTO

UJAUZITO

• • • • • •


Ili kujali usalama wa mama na mtoto aliyeko tumboni,wanawake wajawazito hushauriwa walalie upande wa kushoto au kulia (SOS- Sleep On Side). Katika kuzingatia mazingira ya mfumo wa uzazi wa mwanamke hasa kwenye nyumba ya uzazi ambapo ndipo mtoto huyu hutunzwa,kulalia upande wa kushoto huwa ni bora zaidi kuliko upande wa kulia. 


Husaidia usafirishwaji wa hewa ya kutosha na virutubisho vingi kwenda kwa mtoto kupitia kondo la uzazi. Mapendekezo haya yanaweza yasikupe uhuru mkubwa sana kwa kuwa hukuzoea kabla kulala upande upande,lakini kwa wakati huu ni muhimu sana kuzingatia maana utajitengenezea mazingira mazuri ya wewe kuwa salama nyakati zote


KULALIA MGONGO

Husababisha maumivu makali ya mgongo,kugandamiza mishipa muhimu ya fahamu,bawasiri,presha ya kushuka,choo kigumu,kukata kwa pumzi pamoja na kupungua kwa usambazwaji wa hewa na virutubisho kwenda kwa mtoto. Sababu ya matatizo haya yote ni moja tu, mgandamizo mkubwa hutokea kwenye utumbo na mishipa mikubwa ya damu hasa ile ya Aorta na Vena cava


KULALIA TUMBO

Inaweza pia kutegengeza mgandamizo mkubwa kwa mtoto lakini pia mwanamke mwenyewe hatakuwa na uhuru katika kusinzia!


Hivyo kwa muktadha huu,jitahidi sana ulalie upande wako wa kushoto mara kwa mara bila kujali umri wa ujauzito wako. Unapohisi umechoka unaweza kulalia pia upande wa kulia kwa muda!


 Via @sam_nutritionalclinic




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.