Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

ZIFAHAMU KUCHA ZAKO KWA UNDANI PAMOJA NA MAGONJWA YA KUCHA

ZIFAHAMU KUCHA ZAKO KWA UNDANI PAMOJA NA MAGONJWA YA KUCHA

➡️ Kucha

Nitaanza kutoa maelezo yanayohusu muonekano wa kucha zako na nini maana yake kwenye afya yako. Fuatilia twende sambamba

Tazama kucha zako,muonekano wa aina kama hii inayoonesha kucha ngumu,kavu na zinazovunjika au kujikunja zenyewe tu bila sababu maalumu huhusishwa na matatizo ya tezi za thyroid. Ikitokea kucha hizi zinaonesha tabia hii,kisha zikaenda mbali zaidi kwa kubadilika rangi na kuwa za njano mara nyingi humaanisha uwepo wa maambukizi ya fangasi.

Kumbuka kuwa,tezi za thyroid hufanya kazi kubwa sana ya kuimarisha mifumo ya mwili hasa ile ya ukuaji,kuratibu kazi za mwili pamoja na mfumo wa uzazi kwa jinsia zote,lakini zaidi kwa wanawake. Udhaifu wa tezi hizi katika kusababisha uzalishwaji mwingi au mchache wa vichocheo vyake vya thyroid kunaweza kuleta shida nyingi kwa afya,lakini zaidi ugumba. Chunguza kucha zako,fuatilia uwepo wa fangasi na hakikisha unafuatilia uimara wa tezi zako za thyroid pamoja na vichocheo vyake ikiwa kucha zako zinaonesha tabia hii

?RANGI YA KUCHA ZAKO

• • • • • •

Kucha hazipaswi kuwa na rangi ya manjano kama picha hii inavyoonesha. 

Tazma kucha zako tena,kama zina rangi ya manjano,wasiwasi wa kwanza kabisa ni kuwa una maambukizi ya fangasi. Maambukizi yanapozidi kuwa makubwa,kucha huongezeka unene na mara nyingi huanza kujikunja. Hii ni fangasi

Katika mazingira machache sana,aina hii ya kucha huwa ni dalili muhimu sana kwa watu wenye shida ya kisukari,psoriasis,shida za tezi za thyroid pamoja na uwepo wa ugonjwa au changamoto zozote zile zinazohusisha mapafu. Fanya uchunguzi wa afya yako

Kucha zenye rangi ya blue hutokea kwa watu wanaohama kutoka mazingira yenye joto kwenda kwenye mazingira yenye baridi kali. Kuhakiki jambo hili,mhusika akirudi sehemu yenye joto aliyoizoea,kucha hizi hurudia rangi yake ya kawaida

Ukiachia hali hii isiyo na athari yoyote kwa afya,kucha za blue humaanisha pia kuwa mwili wako haupati hewa ya oxygen ya kutosha hivyo unakabiliwa na upungufu mkubwa wa hewa kwenye damu. Kucha zenye rangi hii zinaweza pia kuwa ni dalili muhimu sana na uwepo wa magonjwa ya moyo,mfumo wa upumuaji na mapafu. Kama unakabiliwa na hali hii,fanya uchunguzi wa afya yako!


?MSTARI MWEUSI KATIKATI YA KUCHA

• • • • • •

Uwepo wa mstari mweusi katikati ya kucha zako siyo ishara nzuri kwa afya yako. Ishara zingine za kucha na maana zake unaweza kurejea kuzitazama (kama hukuona) kwenye post mbili za nyuma

Tazama kucha zako,kama zina muonekano huu zikiwa na mstari mweusi katikati humaanisha kuwa ukucha wako ulipata ajali fulani iliyo sababisha kuvujia kwa damu kwenye sehemu yake ya ndani. Katika mazingira fulani,humaanisha pia uwepo wa saratani ya ngozi,ambayo hutokea baada ya seli za kawaida zinazozalisha vichocheo vinavyoipa ngozi rangi yake kubadilika na kuwa saratani. Huitwa melanoma

?KUNG’ATA KUCHA MARA KWA MARA

• • • • • •

Kung’ata kucha mara kwa mara

Katika nyakati nyingi,kung’ata kucha hutokea bila sababu maalumu. Ni mazoea tu yasiyo mazuri yanayomfanya mhusika aendelee kuzing’ata kila mara zinapochomoza. Hii haina tatizo

Katika nyakati fulani,ung’ataji wa kucha wa mara kwa mara huhusishwa na uwepo wa stress zinazomsumbua mhusika kwa muda mrefu sana ambazo huenda mbali zaidi kwa kusababisha tatizo la akili (ubongo) linaloitwa Obsessive-compulsive disorder (OCD). Hili ni tatizo linalomlazimisha mhusika kufanya au kuwaza kitu fulani (hasa kibaya) kwa kujirudia rudia

Dalili za Obsessive-compulsive disorder (OCD) zipo nyingi,lakini baadhi yake ni kama vile kukagua kagua kitu mara kwa mara hata baada ya kujiridhisha kuwa kipo salama kila siku,kudhani una hali fulani au tatizo fulani kiafya wakati hauna (mfano mwanamke kujihisi mjamzito na kuona dalili zote za ujauzito kumbe hana),kuhisi watu au mtu fulani hakuheshimu na anakuchukulia kama uchafu,kupanga na kupangua muonekano wa vitu fulani mara kwa mara pamoja na wasiwasi kuwa mpenzi wako anakusaliti kumbe hapana

Watu wengine hung’ata kucha wakiwa na msongo wa mawazo,wengine hufanya hivyo wakiwa na njaa!

CR: @ AFYA INFO

.

.

.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Karibu Sana..!!!





Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.