Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA

 SURUALI ZA KUBANA

• • • • • •

MADHARA YATOKANAYO NA UVAAJI WA SURUALI ZA KUBANA 

Watu wengi wamekuwa wakivaa suruali za kubana sana hasa hasa wakina dada,bila kujua pia uvaaji wa suruali za kubana sana una madhara kiafya.

Swala la kuvaa suruali za kubana sana mapaja kwa wadada au wanawake imekuwa fashion kwa watu wengi, na huku baadhi yao wakifikia hatua ya kutokuwa na Nguo nyingine zaidi ya suruali tu.

YAPI NI MADHARA YA KUVAA SURUALI ZA KUBANA SANA?

– Wataalam wa afya wanasema uvaaji wa suruali za kubana sana mapaja ya mtumiaji kwa muda mrefu husababisha tatizo la kukandamiza mshipa wa fahamu ambao hupita eneo la mapajani ambao kwa kitaalam hujulikana kama Lateral femoral cutaneous nerve.

Madhara ya Mgandamizo huu wa mshipa wa fahamu unaopita kwenye eneo la paja la Mtu ni kupata ganzi pamoja na kupata tatizo la kuhisi kuchomwa chomwa kwenye eneo la paja  ambapo tatizo hili kwa kitaalam hujulikana kama Tingling thigh syndrome au Meralgia paresthetica.

USHAURI

• Wataalam wa afya wanapendekeza mtu kuvaa nguo ambazo haziubani sana mwili wake ikiwa ni pamoja na kuacha kabsa tabia ya kuvaa suruali za kubana sana mapaja pamoja na kuvaa viatu virefu sana kwa Muda mrefu.

Kwa kudokeza tu kwa ufupi Madhara ya Uvaaji wa Viatu virefu ni pamoja na;

– kupata maumivu makali ya kiuno na mgongo

– kupata maumivu ya miguu kwenye joint

– kudondoka

– Kupata tatizo la misuli ya mwili kukaza

N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.