Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MATUMIZI YA FLAGYL KUZUIA MIMBA(ukweli wa mambo)

FLAGYL

• • • • •

MATUMIZI YA FLAGYL KUZUIA MIMBA

Je ni kweli kwamba ukitumia flagyl hupati mimba kama wengi wanavyofikiria?

Kuna watu wengi wanaambiana kwamba eti ukitumia flagyl kabla ya kufanya mapenzi basi unajikinga na kupata ujauzito hata ukiwa umeshiriki tendo la ndoa kwenye siku za hatari

TUANZIE HAPA JINSI YA BAADHI YA NJIA ZA UZAZI WA MPANGO HUFANYA KAZI KUZUIA MIMBA

Tuangalie kwanza jinsi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinavyofanya kazi kuzuia mimba, halafu hapo baadae tuangalie na matumizi ya Flagyl kwenye mwili wa binadamu, mwisho tujibu swali letu.

– Moja ya vitu ambavyo njia za uzazi wa mpango hufanya ili kuzuia usipate mimba ni pamoja na;

1. Kuzuia au kupunguza kabsa uwezo wa mayai kutoka katika vifuko vyake yaani kwa kitaalam tunaita Ovulation, kitu ambacho hufanya kuwa vigumu sana kwa mbegu za kiume kukuta yai na kulirutubisha(mimba)

2.Kuongeza uzalishaji pamoja na uzito wa mucus kwenye mlango wa kizazi au tunaita Thickening of cervical mucus, kitu ambacho husaidia kukinga na kuzuia mbegu za kiume kupita kwenye mlango wa kizazi na kulifikia yai la mwanamke

3. Ngozi kwenye Ukuta ambapo mtoto huweza kujishikiza baada ya urutubishaji hufanywa kuwa nyembamba sana kiasi kwamba hata kama yai limerutubishwa ni vigumu sana kijusi kujishikiza hapo na mimba ikaendelea kukua

Soma: Mwanamke Kubeba Mimba baada ya Kujifungua

MATUMIZI YA FLAGYL PAMOJA NA KAZI ZAKE MWILINI

– Flagyl hutumika kutibu magonjwa au maambukizi yanayosababishwa na vimelea jamii ya parasite pamoja na bacteria mbali mbali kwenye mwili wako ikiwemo;

  1. Maambukizi ya Giardia kwenye utumbo mdogo
  2.  Maambukizi ya amiba(amoeba) kwenye utumbo mkubwa
  3. Maambukizi ya bacteria ambayo hujulikana kama Bacteria vaginosis, Trichomonas vaginal infections N.K

MAJIBU YA SWALI LETU

 Je matumizi ya flagyl huzuia mimba?

Majibu; Kutokana na jinsi ulivyoona mchakato wa kuzuia mimba ulivyo pamoja na kazi za Flagyl ulizoziona, ni dhahiri kwamba ni vitu viwili tofauti.

Hivo basi ukweli ni kwamba,matumizi ya Flagyl hayana uhusiano wowote na kukuzuia wewe usipate mimba. 

Hiyo ni dhana tu na imani potofu,

MADHARA YA KUTUMIA FLAGYL ILI KUZUIA MIMBA

Badala ya flagyl kukuzuia usipate mimba kama wengi wanavyodhani, inaweza kukusababishia madhara makubwa kwenye mwili wako hasa pale unapotumia kwa lengo la kuzuia mimba

Na madhara hayo ni kwamba, baada ya kutumia flagyl utapata mimba kama kawaida, na mwisho wa siku huweza kuathiri katika uumbaji wa mtoto, na kukupelekea wewe kuzaa mtoto mwenye matatizo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ulemavu wa viungo

Soma: Mwanamke Kubeba Mimba baada ya Kujifungua

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.