Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA USUBI(chanzo,dalili na tiba)

 USUBI

• • • •

UGONJWA WA USUBI(chanzo,dalili na tiba)

Ugonjwa wa Usubi ni ugonjwa ambao chanzo chake kikuu ni minyoo, hivo ugonjwa huu husababisha na aina ya minyoo ambayo kwa kitaalam hujulikana kama ONCHOCERCA VOLVULUS. Lakini husambazwa kutoka  kwa binadamu mmoja kwenda kwa mwingine baada ya kung’atwa na nzi weusi au Blackflies.

UGONJWA HUU UMEATHIRI MIKOA MBALI MBALI HAPA NCHINI NA MIKOA AMBAYO ILIONEKANA KUWA NA HATARI YA WATU KUPATA UGONJWA WA USUBI NI KAMA VILE;

– Tanga

– Ruvuma

– Iringa

DALILI ZA UGONJWA WA USUBI NI PAMOJA NA;

1. Mgonjwa kupata viupele upele kwenye ngozi yake ya mwili

2. Mgonjwa kupatwa na shida ya upofu wa macho

3. Mgonjwa kupatwa na miwasho ya mara kwa mara kwenye ngozi yake ya mwili

4. Joto la mwili kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa

5. Mgonjwa kukosa hamu ya kula chakula

6. Ngozi ya mwili kuchuchuka

N.K

MATIBABU YA UGONJWA WA USUBI

Moja ya dawa kubwa ambayo hutumika kwa mtu mwenye ugonjwa wa Usubi ni pamoja na  Ivermectin ambayo hutumika kuua Minyoo hii ya ONCHOCERCA VOLVULUS.

Lakini pia njia nyingine ambazo huweza kutumika ni pamoja na upuliziaji wa dawa maalumu kwa ajili ya kuua hawa Nzi weusi au BlackFlies.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.