DALILI ZA MTU MWENYE UPUNGUFU WA VITAMIN D Mwilini
VITAMIN D
• • • • •
DALILI ZA MTU MWENYE UPUNGUFU WA VITAMIN D Mwilini
Katika makala hii tunazungumzia tatizo la upungufu wa vitamin D mwilini yaani kwa kitaalam Vitamin D deficiency. Kwa ujumla, vitamin mbali mbali ni muhimu sana kwenye mwili wako na kila aina ya vitamin ina kazi zake mwilini, hapa nazungumzia mfano; vitamin A, Vitamin B6, Vitamin C, Vitamin D, Vitamin B9, Vitamin B12 n.k
Upungufu wa vitamin D mwilini unasababishwa na nini? Na dalili zake ni zipi?(soma makala hii)
CHANZO CHA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI NI PAMOJA NA;
– Kula vyakula ambavyo havina vitamin D kwa muda mwingi
– Kukaa mbali na jua kwa muda mrefu kwani utengenezaji wa vitamin D mwilini mwako hutegemea pia jua.
– Figo zako kushindwa kubadilisha vitamin D kuwa katika hali ya kutumika zaidi hasa kwa watu wenye umri mkubwa
– Kuwa na ngozi nyeusi sana, tafiti zinaonyesha melanini huweza kupunguza ngozi kutengeza vitamin D pale inapopigwa na jua
– Tatizo la mfumo wako wa umeng’enyaji kushindwa kufyoza vizuri vitamin D mbali na chakula unachokula chenye vitamin vya kutosha.
DALILI ZA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI
– Kupata maumivu ya mgongo mara kwa mara
– Kupata maumivu ya misuli,joint pamoja mifupa ya mwili mara kwa mara
– Kuwa na tatizo la vidonda kutokupona haraka
– Uchovu wa mwili kupita kiasi
– kuwa na tatizo la Nywele kukatika sana na kunyonyoka zenyewe
– Watoto kuwa na shida ya matege
– Kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara kutokana na kinga yako ya mwili kutokufanya kazi vizuri
N.k
TIBA YA UPUNGUFU WA VITAMIN D MWILINI
– Matibabu ya upungufu wa vitamin D mwilini huhusisha matumizi ya vyakula vyenye kiwango cha kutosha cha vitamin D, Dawa zakusaidia umeng’enyaji pamoja na ufyozwaji wa vitamin D mwilini, pamoja na matumizi ya Virutubisho mbali mbali yaani supplements
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.