Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE UPANDIKIZAJI WA VIJITI HUWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA MAPENZI?

 UZAZI

• • • •

JE UPANDIKIZAJI WA VIJITI HUWEZA KUSABABISHA MWANAMKE KUKOSA HAMU YA KUFANYA MAPENZI?


Hili ni swali ambalo baadhi ya Watu hujiuliza sana, Hapa kuna mambo ya msingi unatakiwa kuyafahamu vizuri kabla ya kupata majibu ya Swali hili.


Kijiti ni njia ya Uzazi wa mpango ambayo ina uwezo wa kuzuia mimba kwa kipindi cha Miaka mitatu Pamoja na Miaka mitano.


Ndani ya kijiti hiki kuna vichocheo au Hormones, sasa endapo mtumiaji katumia mpaka hali ya vichocheo vyake vya mwili kuvurugika tatizo ambalo hujulikana kama Hormone Imbalance, hapa ndipo matatizo mengi huanza.


Na kumbuka Moja ya Sababu kubwa ya Mwanamke kukosa hisia za kimapenzi pamoja na Hamu ya tendo la Ndoa ni pamoja na hii ya; Mvurugiko wa vichocheo vyake vya mwili yaani Hormone imbalance


Hivo basi kwa maelezo hayo,tunaweza kusema matumizi ya baadhi ya Njia za uzazi wa mpango kama sindano,vijiti n.k huweza kuchangia mwanamke kukosa hamu ya tendo la ndoa ingawaje hii haiwezi kuwa sababu ya kutosha kusababisha tatizo hili, Zipo sababu zingine nyingi kama vile;


– Uhusiano mbaya kati ya mwanamke na mwanaume huweza kupelekea mwanamke kukosa kabsa hamu ya mapenzi


– Magonjwa mbali mbali kama vile; ugonjwa wa Saratani ya shingo ya kizazi,shinikizo la Damu, maambukizi kwenye via vya uzazi vya mwanamke yaani PID n.k


– Mwanamke kuwa na shida ya kupata maumivu makali kila akishiriki tendo la ndoa, hali ambayo humsababishia hofu, kutokufurahia mapenzi na hata kukosa kabsa hamu ya tendo la ndoa.


– Matatizo ya Kisaikolojia au Mwanamke kuathirika kisaikolojia


– Mwanamke kuwa na tatizo la msongo wa mawazo


– Mwanamke kupata majeraha yoyote yale sehemu za siri yanayotokana na sababu mbali mbali kama vile kubakwa n.k


– Matumizi ya baadhi ya Dawa

N.K


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.