Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO(kitovu kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa)

KITOVU

• • • •

JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO(kitovu kinaweza kuwa chanzo cha magonjwa)

Bila shaka wewe ni shahidi kwamba ukiangalia vizuri kitovu kama hujakisafisha vizuri utaona kuna mabaki ya uchafu yapo pale.

Mabaki yale huweza kutengeneza mazingira mazuri ya bacteria mbali mbali kuanza kuzaliana.

FAHAMU HII; Kuna utafiti ulifanyika mwaka 2012 kutoka kwa wataalam mbali mbali wa afya, ukaonyesha kwamba kuna wastani wa aina 67 za bacteria ambao huweza kupatikana kwenye kitovu chako bila wewe kujua.

HAKIKISHA UNASAFISHA KITOVU CHAKO VIZURI,

Bila shaka watu wengi,moja ya eneo ambalo hawalizingatii sana wakati wanafanya usafi wa mwili au kuoga ni pamoja na Kitovu,

Lakini je wajua? Sehemu hii ni muhimu sana kuzingatia,

Tafiti zingine zinaonyesha kwamba, Eneo hili huweza kuhifadhi bacteria zaidi ya aina 70,

Lakini pia eneo hili huweza kutoa harufu mbaya bila wewe kujua.

Hakikisha hulisahau eneo hili wakati wa kufanya usafi wa mwili au wakati wa Kuoga.

Watu wengi wakishaoga husafisha mwili mzima bila kujali kitovu kipo safi au kipoje, lakini nikukumbushe kwamba usafi wa kitovu ni muhimu sana kuliko unavyofikiria.

Unaweza kuanza kuchunguza kitovu chako sasa na endapo ukaona kuna uchafu basi tumia njia hii hapa kujisafisha.

JINSI YA KUSAFISHA KITOVU CHAKO

Vifaa;

  1. Unatakiwa uwe na Dettol
  2. Unatakiwa uwe na kibeseni kidogo ambacho kina maji yaliyochanganywa na dettol
  3.  Unatakiwa uwe na kibeseni kingine cha maji safi
  4. Unahitajika uwe na vipisi 3 vya pamba au kitambaa kidogo sana kisafi ambacho huweza kupenya vizuri kwenye kitovu chako

KISHA FANYA YAFUATAYO;

✓ Weka kipisi cha kwanza cha pamba au kitambaa kidogo kisafi kwenye maji yaliyochanganywa na dettol kisha safisha kwa kuingiza ndani na kuzungusha ndani ya kitovu taratibu ili kuhakikisha unatoa uchafu wote nje, baada ya uchafu kutoka

✓ Chukua kipisi cha pili cha pamba au kitambaa safi kiweke kwenye maji masafi ambayo hayajawekwa chochote kisha tumia njia kama ya mwanzoni ya kuingiza ndani ya kitovu pamoja na kuzungusha vizuri taratibu

✓ Kisha malizia kwa kuchukua kipisi cha mwisho cha pamba au kitambaa kidgo safi ambacho ni kikavu pitisha tena kwa kuingiza ndani na kuzungusha tararibu vizuri.

Mpaka hapo kitovu chako kitakuwa safi, baada ya hapo kuwa muangalifu na kujali kitovu chako kila mara unaposafisha mwili wako.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.