Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

SABABU ZA MTU KUKONDA

SABABU ZA MTU KUKONDA

sababu za mtu kukonda kuweza kuwa za moja kwa moja au mwingine huweza kukonda bila kujua sababu hasa ni nini.

Katika makala hii tunachambua baadhi ya sababu ambazo huweza kusababisha mtu kukonda sana.

SABABU ZA MTU KUKONDA NI PAMOJA NA;

✓ Mtu kufanyiwa operation ya kukata utumbo, Operation hii husababisha mtu kula chakula kidogo sana na kuhisi kushiba kwa haraka au kutokula kabsa hali ambayo hupelekea matatizo mbali mbali mwilini kama Utapiamlo,uzito kupungua sana na mtu kukonda sana.

✓ Mashambulizi ya magonjwa mbali mbali kama vile ugonjwa Wa Kisukari n.k

✓ Kupata lishe duni sana, Moja ya sababu kubwa ya mtu kukonda ni kula vyakula ambavyo havina kabsa virutubisho vya kujenga mwili kama proteins za kutosha n.k

✓ Mtu Kuwa na tatizo la kutapika kupita kiasi kila anapokula chakula, hali hii huweza kumsababisha mtu kukonda kupita kiasi ndani ya muda mfupi tu

✓ Mtu kupata tatizo la kuharisha mfululilo kwa muda mrefu

✓ Kuwa na Tatizo la minyoo iliyokithiri

✓ Mtu mwenye tatizo la upungufu wa kinga mwilini yaani UKIMWI

✓ Mtu kukosa muda wa kulala kabsa na kupumzika kutokana na kazi nyingi anazofanya,mara nyingi afya yake hudhorota sana

✓ Kuwa na Tatizo la Msongo wa mawazo ambao hauishi

✓ Kuwa na hofu na wasiwasi wa maisha, mbali na kwamba hofu huweza kushusha kinga yako ya mwili, hata kukonda pia unaweza kukonda.

✓ Kukaa na Njaa kwa muda mrefu, Huku wengine wakiacha kula baadhi ya milo kwa siku.

✓ Matumizi ya baadhi ya Dawa

n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.