Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MSHIPA WA KORODANI ZA MWANAUME KUBANA NA KUSOKOTA(testicular torsion)

 AFYA KWA WANAUME

• • • • • 

TATIZO LA MSHIPA WA KORODANI ZA MWANAUME KUBANA NA KUSOKOTA(testicular torsion)


Testicular torsion ni tatizo ambalo huhusisha korodani zenyewe kuzunguka kusiko kawaida hali ambayo huweza kusababisha mishipa inayopeleka damu kwenye korodani kusokota,kubana na kuathiri upelekaji wa damu kwenye korodani.


CHANZO CHA TATIZO HILI


– Chanzo cha tatizo la Testicular torsion ni kuzunguka kusiko kwa kawaida kwa korodani na kusababisha mishipa ya damu ndani ya korodani kusokota,kubana pamoja kuziba kabsa,hali ambayo huathiri mtiririko wa damu kwenye korodani.


Hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa hali hii japo zipo baadhi ya sababu ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii kama vile;


✓ Umri, watu ambao wana umri wa miaka 12 na 18 wapo kwenye hatari zaidi, japo shida hii huweza kutokea kwa mtu wa umri wowote hata mzee,kijana au mtoto ambaye bado hajazaliwa


✓ Kuwa na historia ya tatizo hili siku za nyuma, upo kwenye hatari ya tatizo kurudi tena


✓ Kuwa na mtu mwenye shida hii kwenye familia au koo


DALILI ZA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


1. Mwanaume kuanza kupata maumivu ya gafla ya Korodani


2. Mwanaume kupata maumivu makali ya tumbo


3. Mwanaume kuanza kupata shida ya korodani kuvimba


4. Korodani ambayo imeathirika kushuka chini zaidi kuliko nyingine


5. Mwanaume kukojoa mara kwa mara


6. Joto la mwili kwa Mgonjwa kuwa juu au mgonjwa kuwa na homa


7. Kupata kichefu chefu na kutapika mara kwa mara


8. Mwanaume kupata maumivu makali ya korodani wakati wa tendo la ndoa na baada ya tendo la ndoa


MATIBABU YA TATIZO HILI NI PAMOJA NA; 


– Wataalam wa afya kutumia njia ya mbali mbali kama dawa, njia ya kutumia mikono kurudisha korodani kwenye hali yake ya kawaida pamoja na njia ya upasuaji.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.




Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.