Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA FIZI(chanzo,dalili na tiba yake)

 FIZI

• • • • •

UGONJWA WA FIZI(chanzo,dalili na tiba yake)


Huu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya fizi na huhusisha matokeo mbali mbali kama vile kuvimba kwa fizi, Fizi kutoa damu, Fizi kuuma N.K


CHANZO CHA UGONJWA WA FIZI


– Mtu kushambuliwa na magonjwa mbali mbali ambayo huathiri tisu za meno maarufu kama Periodontal disease


– Mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile; Bacteria N.K


– Kuumia kwa tisu za meno au fizi kutokana na sababu mbali mbali kama vile; Kuchomwa na kitu cha ncha kali N.K


– Mtu mwenye ugonjwa wa kisukari ambao ni ngumu kuudhibiti yupo kwenye hatari pia ya kupatwa na magonjwa ya Fizi


DALILI ZA UGONJWA WA FIZI NI PAMOJA NA;


1. Mgonjwa kupata maumivu makali ya kwenye fizi hasa wakati wa kula kitu chochote.


2. Fizi za mgonjwa kutoa damu.


3. Fizi za mgonjwa kubadilika rangi na kuwa nyekundu sana kuliko kawaida.


4. Mgonjwa kupatwa na shida ya Fizi kuvimba.


5. Kuwa na vidonda au michubuko kwenye ngozi ya fizi.

N.K


MATIBABU YA UGONJWA WA FIZI


– Zipo dawa mbali mbali ambazo hutumika kutibu ugonjwa huu japo hutegemea chanzo cha ugonjwa huu.


Hivo ni vizuri mgonjwa kwenda hospital kwa ajili ya uchunguzi kwa kina pamoja na kupata matibabu sahihi kwake.


KUMBUKA; Usafi wa kinywa ni muhimu sana ili kusaidia kuondoa uchafu wa chakula au mabaki ya chakula, kusaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni pamoja na kukukinga na magonjwa mbali mbali ya Fizi.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.