Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE(afya ya mifugo)

AFYA YA MIFUGO
• • • • • •
UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE(afya ya mifugo)

Ugonjwa wa homa ya nguruwe ni ugonjwa ambao husababishwa na vimelea vya magonjwa jamii ya Virusi na kushambulia Nguruwe.

 
 Ugonjwa huu wa homa ya nguruwe umeua nguruwe wengi sana na kwa haraka zaidi kuliko magonjwa mengine katika maeneo mbali mbali ya dunia.
 
NB; Ugonjwa huu wa homa ya nguruwe hushambulia na kuathiri zaidi maeneo haya katika mwili wa nguruwe; Mfumo mzima wa damu, Mfumo wa chakula, pamoja na Mfumo wa upumuaji.
 
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE NI PAMOJA NA;
 
1. Joto la mwili wa nguruwe kuwa juu sana au nguruwe kuwa na homa
 
2. Nguruwe kukosa kabsa appetite ya chakula, hivo hata ukimpa chakula nguruwe hataki kula
 
3. Vifo vya gafla kwa nguruwe wengi
 
4. Nguruwe kunyong’onyea sana
 
5. Nguruwe kutoa damu kwenye maeneo mbali mbali ya mwili wake kama vile masikioni,puani N.K
 
6. Nguruwe kulala lala kila mara
 
7. Nguruwe kupata shida ya upumuaji
 
8. Rangi ya ngozi kwa nguruwe kubadilika na kupauka zaidi
9. Nguruwe kuharisha kinyesi kilichochanganyika na damu
 
10. Eneo la matakoni kubadilika rangi na kuwa jekundu zaidi
 
11. Nguruwe kupatwa na hali ya kikohozi kila muda
 
MATIBABU YA UGONJWA WA HOMA YA NGURUWE
 
– Mpaka sasa bado hakuna tiba ya moja kwa moja kwa ajili ya kutibu ugonjwa huu, Matibabu ya homa ya nguruwe yapo katika kudhibiti dalili mbali mbali za ugonjwa huu.
 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.