Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha Mtu Kupiga CHAFYA,Tiba yake na Faida zake

Chanzo cha Mtu Kupiga CHAFYA na Faida zake

Kwa namna moja au nyingine kupiga chafya huweza kuwa ni mojawapo ya Njia ya mwili kuondoa uchafu au kitu chochote ambacho kinajaribu kuingia kwenye njia ya hewa,

japo zipo sababu mbali mbali zinazochangia mtu Kupiga Chafya.

SABABU ZA MTU KUPIGA CHAFYA NI PAMOJA NA;

– Tatizo la allergy juu  ya vitu flani kama sabuni,mafuta,perfume n.k

– Tatizo la mashambulizi ya Virusi wanaosababisha mafua kama vile; maambukizi ya RHINOVIRUS n.k

– Kuingia kwa vitu vya kigeni kama Vumbi, Pilipili n.k ambavyo husababisha hali ya muwasho ndani ya pua

– Mtu kuacha gafla matumizi ya dawa kama vile; Opioid narcotics

– Kuvuta dawa puani jamii ya Corticosteroids

– Kuvuta hewa ya baridi sana

– Na mara chache sana kuumia ndani ya pua

n.k

MATIBABU

endapo kupiga chafya imekuwa tatizo la kila mara, ni muhimu kuepuka vitu ambavyo hukusababishia tatizo lako,

Au unaweza kuongea na wataalam wa afya kwa ajili ya msaada zaidi.

KUMBUKA; Kupiga chafya kuna Faida mwilini,lakini kunaweza kuwa ni ugonjwa pia ambao huhitaji tiba

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.