Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

DAWA YA KUNG’ATWA NA NYUKI(huduma ya kwanza)

 NYUKI

• • • • •

DAWA YA KUNG’ATWA NA NYUKI(huduma ya kwanza)

Fahamu kuhusu huduma ya kwanza pamoja na matibabu kwa mtu ambaye ameng’atwa na nyuki,

Kwanza hakikisha wewe unayeenda kumsaidia mtu aliyeng’atwa na nyuki unajilinda kwanza, kwa kuvaa nguo ambazo zinafunika mwili wako wote,

Kisha angalia hali ya mtu aliyeng’atwa na nyuki, kama bado nyuki wapo wengi na wanaendelea kumng’ata fanya haya;

– Unaweza kumfunika mwili wake wote kwa blanket nzito

– Kumwagia maji mwilini ili kuondoa harufu ya nyuki mwilini 

– Tumia kitu chembamba sana kuondoa ile miiba ya nyuki sehemu ambapo kang’atwa, usitoe kwa kutumia kucha zako,ni rahisi sumu ile kuendelea kupenya kwenye ngozi na kuingia mwilini

– Muweke aling’atwa na nyuki sehemu ambapo kuna hewa ya kutosha

– Wengine hutumia mafuta ya kupaka kama Calamine n.k

– Tumia dawa mbali mbali za kuzuia maumivu 

– Baada ya muda tumia maji safi na sabuni kuosha sehemu ambazo kang’atwa na nyuki

– Endapo hali ya mgonjwa ni mbaya zaidi,mpeleke kwenye hospital iliyokaribu na wewe ili apate matibabu zaidi

MADHARA YA KUNG’ATWA NA NYUKI

NYUKI huweza kusababisha;

– Hali ya kuvimba sana mwilini

– Mtu kupoteza kabsa fahamu

– Mwili kuwasha sana

– Maumivu makali sana

– Mtu kupoteza maisha

– Maumivu makali ya kichwa

– Kizunguzungu kikali

– Mapigo ya moyo kubadilika na kwenda mbio sana kuliko kawaida

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.