Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

JE UNAWEZA KUISHI NA FIGO MOJA BILA MADHARA YOYOTE?

 FIGO

• • • • •

JE UNAWEZA KUISHI NA FIGO MOJA BILA MADHARA YOYOTE?

Kabla ya kujibu swali hili, fahamu kwamba kuna baadhi ya watu huzaliwa na Figo moja na maisha yanaendelea kama kawaida,

Je kuna madhara yoyote mtu akiwa na Figo moja?

Hakuna madhara yoyote ya mtu kuwa na figo moja, kitu cha msingi sio idadi ya figo ulizonazo, Kitu cha msingi ni uwezo wa Figo yako kufanya kazi vizuri bila matatizo yoyote.

MUHIMU; Kama una figo moja unachotakiwa kukifanya ni kuilinda sana kwa sababu huna nyingine, na ulinzi huo ni pamoja na Kufanya mambo yafuatayo;

✓ Kuacha matumizi ya pombe kabsa

✓ Kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote na kuepuka kula vyakula vya mafuta sana

✓ Kufanya mazoezi ya mwili

✓ Kuhakikisha uzito wako unakuwa wa kawaida na kuepuka matatizo kama unene au uzito kupita kiasi

✓ Epuka matumizi ya Dawa hovio

✓Hakikisha shinikizo lako la damu linakuwa kwenye hali nzuri au hali ya kawaida

✓ Epuka hali ya msongo wa mawazo kwa muda mrefu

✓ Jenga utaratibu wa kufanya checkup mara kwa mara,sio mpaka uumwe

N.k

KUMBUKA: Ukiwa na Figo Moja unakuwa kwenye hatari zaidi ya kupata matatizo ikiwemo figo yenyewe Kufeli,kama Usipokuwa makini sana hasa kwenye mtindo wako wa maisha ikiwemo Ulaji wako.

Kama Umezaliwa na figo Mbili,ni vizuri kuzitunza Zote, Lakini kwa Wale ambao pia huchangia figo kwa Watu wao wa karibu kutokana na matatizo ya Kiafya,Unashauriwa kupata maelekzo kwa kina Kutoka kwa wataalam wa afya kabla ya kufanya Hivo.

#Uhaikwanza #Maishakwanza

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

2 Comments

  1. Hello,am Godson Sagga,from Iringa.My young brother is suffering from such problems,its happened that all of his kidneys are not functioning.And the dialysis is very costful.Insteady we need such cancelling.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.