Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya kuinama kwa mjamzito(dalili za hatari kwa mwanamke mjamzito)

 MJAMZITO

• • • •

Madhara ya kuinama kwa mjamzito(dalili za hatari kwa mwanamke mjamzito)

FAHAMU:

Kunyanyua vitu vizito sana, Kusimama kwa muda mrefu sana, Kujikunja sana,kutikiswa sana ikiwa ni pamoja na kuinama sana na kwa Muda mrefu,

huongeza uwezekano wa kutoka kwa ujauzito yaani Miscarriage, mwanamke mjamzito kujifungua kabla ya wakati yaani Preterm birth, Au kupata majeraha.

KUMBUKA: Kwa Mwanamke mwenye shida ya mimba au Ujauzito kutoka mara kwa mara,ni muhimu sana kuepuka kufanya kazi ngumu na kupata muda wa kutosha wa kupumzika (bed rest),

Hii itamsaidia kujikinga na madhara kutokea tena kwenye ujauzito wake

DALILI ZA HATARI KWA MWANAMKE MJAMZITO

Mwanamke mjamzito hushauriwa kuwahi haraka hospital endapo atapata dalili hizi hapa chini;

– Kuvuja damu sehemu zake za siri

– Kutoa maji sehemu za siri

– Kutoa uchafu wenye harufu mbaya sana ukeni

– Kutokumsikia mtoto akicheza tumboni zaidi ya masaa 24 kwa wale ambao mtoto kafikia umri wa kucheza tumboni

– Mwanamke mjamzito Kuona marue rue

– Kuvimba kupita kiasi miguuni,kwenye mikono,usoni n.k

– Joto la mwili kupanda au mama mjamzito kuwa na  Homa

– Mwanamke mjamzito kupata kizunguzungu

– Kuanza kuwa na mawazo ya kutaka kujiua mwenyewe au kuuwa kiumbe kilichopo tumboni

– Kupata maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu

– Kupata maumivu makali sana ya kichwa

n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.