Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA MOYO KUJAA MAJI(chanzo,dalili na Tiba)

 MOYO

• • • • • •

TATIZO LA MOYO KUJAA MAJI(chanzo,dalili na Tiba)


Tatizo la moyo kujaa maji ni mojawapo ya matatizo ambayo ni hatari zaidi kwani mtu asipopata matibabu huweza kupoteza maisha,


Tatizo hili hutokea pale ambapo kuta za kwenye moyo yaani Pericardium zimepata jeraha,kuumizwa, au kupata maambukizi ya magonjwa mbali mbali,


Hali ambayo hupelekea moyo kushindwa kufanya kazi vizuri kama ilivyokawaida.


CHANZO CHA TATIZO LA MOYO KUJAA MAJI


– kuvimba kwa kuta ndani ya moyo yaani Pericardium, kutokana na sababu mbali mbali kama vile; maambukizi ya magonjwa, majeraha n.k


– Maambukizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa ndani ya moyo mfano; maambukizi ya bacteria kama vile Staphylococcus, pneumococcus na streptococcus,


Maambukizi ya virusi mbali mbali kama vile; Virusi vya ukimwi n.k


– Mtu kuwa na tatizo la majeraha au kuumia ndani ya moyo


– Mtu Kupatwa na tatizo la mashambulizi ya Kansa mbali mbali mfano; kansa ya matiti,kansa ya mapafu n.k


– Mtu kupatwa na tatizo la moyo kufeli kusukuma damu yaani Heart failure

n.k


– Mtu kupatwa na tatizo la shambulio la moyo yaani heart attack, pamoja na kwa kiasi kidogo kwa watu wenye tatizo la figo kufeli


DALILI ZA TATIZO LA MAJI KUJAA KWENYE MOYO NI PAMOJA NA;


✓ mtu kupata tatizo la kushindwa kupumua na kukosa pumnzi


✓ mtu kupata maumivu makali ya kifua


✓mwili kuchoka kupita kiasi


✓ mtu kupata shida sana pale anapolala


✓ mtu kuhisi kifua kizito na kujaa kuliko kawaida

n.k


MATIBABU YA TATIZO LA MOYO KUJAA MAJI


– Matibabu ya tatizo la moyo kujaa maji hutegemea na chanzo chake pamoja na hali ya mgonjwa,


Kama mgonjwa anaendelea vizuri,basi mgonjwa hupewa dawa mbali mbali kulingana na chanzo cha tatizo kama vile; dawa jamii ya antibiotics kwa ajili ya mashambulizi ya bacteria,dawa kwa ajili ya virusi yaani Antiviral drugs, dawa za kushusha uvimbe,dawa za maumivu n.k


Lakini kama mgonjwa yupo kwenye hali mbaya zaidi, huweza kufanyiwa upasuaji wa moyo na kuvutwa maji yote yaliyojaa ndani ya moyo.


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.