Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)

 Q FEVER

• • • • •

UGONJWA WA Q FEVER(chanzo,dalili,madhara na Tiba)


CHANZO


Ugonjwa wa Q fever ni ugonjwa ambao husababishwa na bacteria wanaojulikana kwa jina la Bacterium Coxiella Burnetii,


Bacteria hawa husambazwa kwenda kwa binadamu kupitia wanyama kama vile; Mbuzi,kondoo n.k


DALILI ZA UGONJWA WA Q FEVER NI PAMOJA NA;


✓ Joto la mwili kuwa juu sana Mfano; 41 °C


✓ Mgonjwa kupata tatizo la kuharisha


✓ Kupata kichefuchefu pamoja na kutapika


✓ Mgonjwa kukohoa mara kwa mara


✓ Mwili kutetemeka


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Mgonjwa kupata maumivu makali ya Kichwa



MADHARA YA UGONJWA WA Q FEVER


– Ugonjwa huu huweza kuharibu Mapafu,Ubongo,Ini pamoja na Moyo


– Ugonjwa huu huweza kusababisha kuvimba kwa kuta za ndani ya moyo yaani kwa kitaalam Endocarditis


– Ugonjwa huu huweza kusababisha shida kwenye mapafu kama vile; Pneumonia n.k


– Ugonjwa huu huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwenye ujauzito kama vile;mimba kutoka zenyewe,mtoto kuzaliwa kabla ya wakati(premature), mtoto kuzaliwa na uzito mdogo,mtoto kuzaliwa mfu n.k


MATIBABU YA Q FEVER


• Ugonjwa huu huweza kutibiwa kwa kutumia dawa mbali mbali kama vile; Doxcycline n.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.